Pages

Monday, June 4, 2012

Lady Jaydee ni mtu wa tatu maarufu zaidi Tanzania kwenye mtandao

Mtandao huo uliozinduliwa rasmi juzi (May 31) ni mkubwa zaidi wa aina hiyo wenye uwezo wa kusoma tabia za watu bilioni 1.5 duniani kote.
Charts hizo zinajumuisha mambo yote kuanzia makampuni, wanamichezo, wanamuziki, vyombo vya habari n.k na kuviweka pamoja kwenye chart ambayo hubadilika kila siku.
Kwa leo Jaydee amekamata pia nafasi ya 34 kwa umaarufu mtandaoni kwa upande wa Afrika Mashariki na kwa dunia nzima amekamata nafasi ya 19,062.
Katika chart hiyo upande wa Tanzania nafasi ya pili imekamatwa na Hasheem Thabeet, nafasi ya nne ni mtandao wa Jamii Forums, (5) Mwananchi Communications, (6) Rais Jakaya Kikwete, (7) Air Tanzania, (8) ZanAir, (9) Michael Mlingwa, (10) Muhidin Issa Michuzi