Pages

Thursday, June 21, 2012

MALIPO YA FIDIA MBAGALA KUU KUANZA KUTOLEWA JUNI 25


Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bw. Mecky Sadiq akitoa taarifa kwa umma juu ya malipo ya fidia kwa ajili ya malalamiko ya fidia ndogo huko Mbagala ambapo amefafanua kuwa zoezi hilo litaanza mtaa wa Mbagala Kuu tarehe 25/6/2012 na kuwa litaendelea na mitaa mingine inayohusika.

Serikali ya Tanzania imewataka wananchi waliokuwa na malalamiko na yakafanyiwa tathmini kufika katika ofisi za kata au mitaa yao kuona majina yao kwa ajili ya malipo.

Akitoa taarifa hii leo jijini Dar es Salaam Mkoa wa Mkoa Bw. Mecky Sadiq amesema wahusika watakaoona majina yao wanatakiwa kwenda na vitambulisho na kumbukumbu walizonazo zitakazowezesha dawati la malipo kufanya kazi yake kwa urahisi.

Amesema Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke atatoa matangazo kwa njia ya vipaza sauti kwenye maeneo husika kuwafahamisha wananchi juu ya zoezi hilo.

Tathmini iliyofanyika ilikuwa ni kwa wananchi 2,132 waliokuwa na madai ya kiasi cha Tsh. 2,236,037,741/- na baada ya kupitiwa upya na uhakiki kufanyika jumla ya wananchi 1,788 imethibitisha kustahili malipo hayo yenye jumla ya Tshs. 2,200,000,000/-.

Madai ya wananchi 344 waliokuwa na madai yao ya Tshs. 36,037,741/- yamebainika kutostahili kwa sababu mbalimbali.