Pages

Wednesday, June 6, 2012

UNGENIUMIZA - Q CHIEF

Unaweza ukajiuliza sana kwanini Q-Chief alikuwa kwa muda mrefu kidogo ametulia kabla ya kuanza kuachia “mabomu” takribani tangu mwaka jana hivi.Nasema unaweza ukajiuliza kwa sababu kwa mapana Q anaweza.Ana kipaji na pengine kama alivyowahi kuniambia katika mahojiano baina yangu naye miaka ya nyuma kidogo, yeye ni tajiri wa sauti. Lakini pengine tusijiulize sana.Si tushawahi kusikia habari za kimya kingi kina mshindo mkuu?Huenda.Au wewe unasemaje?Husikii? Hapa ni wimbo mpya kutoka kwa Q-Chief ambaye pia anajulikana kama Q-Chilla achilia mbali majina mengine aliyojipachika mwenyewe kama vile Savimbi nk.Wimbo unaitwa Ungeniumiza. Can you relate to this song?Ukachungulia mbele ya safari ukaona kiza kitupu.Unapotoka ni karibu kuliko unapokwenda.Ukaona isiwe tabu,ngoja niishie hapa.Ni mapenzi yenye upofu na kisha kama vile Mwana wa Yule Mnazareti alivyokuwa akigusa watu wakaona tena,na wewe huyooo,ghafla unaona tena.Maisha.Msikilize Q-Chief hapa