BABA
mzazi wa nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’, (pichani)
Abdul Juma ameibuka ambapo mbali na tukio hilo pia amenena mambo mazito
kuhusu mwanaye huyo huku akimsukumia tuhuma nzito mama mtu, Amani
linaanika kila kitu.
ASAKWA PANDE ZOTE ZA DAR
Awali
lilitangulia zoezi la kumsaka baba Diamond katika pande zote za Jiji la
Dar es Salaam ili kumsikia alichonacho moyoni kuhusu mafanikio ya
mwanaye huku taarifa za mahali anapoishi zikipotoshwa na watoa habari
wetu.
Wapo waliosema mzee huyo anaishi Kibamba, wengine Mbagala, pia wapo waliodai anakaa Manzese au Magomeni, jijini Dar es Salaam.
Timu
ya mapaparazi wa Amani ilizama kazini kikamilifu ikiapa kumnasa mzazi
huyo popote alipo na hatimaye Julai 2, 2012 saa saba mchana ilifanikiwa
kupabamba nyumbani kwake, Magomeni Kagera, jijini Dar es Salaam lakini
mwenyewe hakuwepo.
Ziliachwa salamu za utambulisho kwa jirani mmoja ili atakaporudi mzee huyo amtaarifu kuwa mapaparazi watarudi siku nyingine.
Julai
7, 2012 saa tano asubuhi mapaparazi wetu walitinga nyumbani hapo na
kumkuta mzee huyo akisema alipata salamu na alikuwa akisubiri ujio huo,
hivyo akawa amejiibua mwenyewe.
AANZA KWA KUANIKA HISTORIA KWA UFUPI
Baada
ya salamu na utambulisho, mzee huyo alianza kwa kukiri kwamba kweli
yeye ni baba mzazi wa Nasibu (Diamond) na kuweka wazi kwamba aliachana
na mama mzazi wa msanii huyo miaka 9 iliyopita.
“Ni
kweli mimi ndiye Abdul Juma, ni baba mzazi wa Nasibu au Diamond. Eee,
mimi niliachana na mama Nasibu miaka tisa iliyopita, tena siku
tunatengana niliondoka nyumbani saa tisa usiku, maana nilikuwa naishi
kwao (ukweni).
AMGEUKIA DIAMOND
Kinyume
na matarajio ya kuzungumzia mafanikio ya mwanaye kwa sasa, baada ya
kuwekwa katikati na waandishi wetu, mzee Abdul ‘aliangusha’ kilio cha
lawama kwa Diamond kuhusu matendo anayomfanyia kila kukicha.
Mzee
huyo anayeonekana ‘kisharobaro’ alisema mafanikio makubwa aliyonayo
mwanaye yasimfanye ashindwe kumthamini yeye kama baba na mapenzi yake
kuyaelekeza kwa mama yake tu.
“Kuhusu
Diamond, labda nimwambie huyu mtoto kuwa, amepata mafanikio ndiyo,
lakini mafanikio hayo yasimfanye ashindwe kunithamini mimi kama baba
yake na kupeleka mapenzi yote kwa mama yake tu,” alisema.
NI KWANINI?
“Nasema
hivyo kwa sababu, zamani kabla jina lake halijawa kubwa, mawasiliano
yetu yalikuwa mazuri sana, lakini nikaja kushangaa baada ya kuwa staa,
akakata mawasiliano na mimi baba yake, aliangalie hilo.”
Akaongeza: “Sisemi kwa sababu nataka awe ananiletea hizo fedha zake, la hasha! Ila mimi kama baba yake ajue kuniheshimu.
“Diamond
nampigia simu hapokei, namtumia meseji hajibu, maana yake nini?
Naumizwa sana na kitendo cha kutopokea simu yangu kila ninapompigia
kumjulia hali. Na hali hii ameanza mara baada ya kupata mafanikio.
JARIBIO
LAIVU Katika kuthibitisha hilo, paparazi wetu alimtaka mzee huyo
kumwendea hewani mwanaye ili kujiridhisha kama kweli ‘hapokeagi’ simu
yake, simu ikapigwa, ikaita wee mpaka ikakatika.
Baba Diamond: “Si umeona, si nilikwambia ukawa huamini.”
MARA YA MWISHO KUMUONA DIAMOND
Mzee
huyo aliendelea kutiririka kuwa, mara ya mwisho Diamond kufika nyumbani
kwake ilikuwa mwezi wa tatu (Machi) mwaka huu baada ya hapo mawasiliano
yakakatika.
“Diamond
alikuja nyumbani kwangu mwezi wa tatu ikiwa ni mfungo wa tatu katika
dini yetu ya Kiislam, akanipa fedha. Baada ya hapo hatujaonana tena wala
hanijulii hali,” alilalama mzee wa watu.
SMS YA MWISHO KUIJIBU
Alisema
Aprili, mwaka huu, Diamond alipotwaa tuzo tatu za Kili Music Awards
2012, yeye alimtumia ujumbe mfupi wa maneno akimpa hongera naye akajibu
asante baba. Lakini baada ya hapo ikawa imetoka.
“Baada
ya kufanikiwa kutwaa tuzo za Kili, mwaka huu nilimpigia simu mwanangu
ili nimpongeze, hakupokea, nikamtumia SMS ndipo akajibu, ‘asante baba’,
mchezo ukaishia hapo.
“Namshukuru
sana dada yake, Mwajuma Abdul (Queen Darleen) yeye ndiyo yupo karibu
sana na mimi kwani mara kwa mara anakuja kunitembelea na wakati mwingine
hunikumbuka kwa fedha, hata pale aliposhinda tuzo ya Wimbo Bora wa
Dancehall alifika nyumbani kunionesha tuzo yake, binafsi nilijisikia
furaha,” alisema mzee Abdul ambaye kwa sasa hana mke.
HAJUI ANAPOISHI MWANAYE
Mbali na msanii huyo kutopokea simu ya baba yake kila anapompigia, vile vile mzee huyo alidai hajamuonesha wapi anapoishi.
“Huyu
mtoto hajawahi kunionesha anapoishi, sijui anafikiri nikiwa karibu naye
nitakuwa namuomba fedha. Mimi sina njaa ‘kihivyo’ na wala sitaki fedha
zake, ila ninachotaka salamu tu, nasikiasikia anaishi Mwenge (usahihi ni
Sinza Mori) lakini hataki kunionesha.
“Ninachojua
yote haya yana mwisho kwani nyota aliyonayo sasa kuna siku itazima.
Simuombei mabaya lakini inaniuma sana kunifanyia hivyo.”
DIAMOND APIGIWA SIMU MARA KUMI NA MBILI
Baada
ya kupata matamshi hayo ya baba mzazi wa Diamond, mwandishi wetu siku
ya Jumanne alifanya jitihada za kumpata msanii huyo ili ajibu
‘mashitaka’ hayo lakini licha ya kupigiwa simu mara kumi na mbili
hakupokea.
Mbali
na kupigiwa simu, paparazi wetu alimtumia ujumbe mfupi wa maneno
kupitia simu yake ya mkononi, lakini pia hakujibu kitu. Juhudi za
kumsaka zinaendelea.
Source: GPL