|
Hivi ndivyo gari la Chege lilivyokuwa baada ya ajali |
Msanii wa Kigoma All Stars Chege Chigunda usiku wa jana amepata
ajali mbaya ya gari maeneo ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Taarifa za awali kuhusu ajali hiyo zimesema kuwa usiku
huo Chege alikuwa ametokea jijini Nairobi.
Chege amesema usiku huo wa saa nne akiwa kwenye gari alikutana
pikipiki katika mtaa mmoja wa maeneo ya Temeke ambaye alimgonga na yeye kupata
ajali hiyo.
Chege amepata majeraha kadhaa lakini anaendelea vizuri
licha ya gari lake kuharibika vibaya maeneo ya mbele.
Haikuweza kufahamika mara moja hali ya mtu huyo aliyekuwa na
pikipiki.
NAHUU NI UJUMBE KUTOKA KWA CHEGE : habari jamani!taarifa zinazosambazwa sio nzuri!mimi nimepata ajali kubwa
sana jana bt nashkuru nimepona kbs,jamaa wa bodaboda alikua amepora
pikipiki ya watu,na alikua amelewa sana so baada ya ajali alivunjika
mguu kbs na bodabaoda imekatika yote gari yangu pia imekufa kabisa bt
namshkuru mungu uhai bado ninao!huo ndio ukweli kamili