Pages

Friday, July 6, 2012

Jason Derulo kumfanyia ‘birthday party’ Ambwene Yesaya




Jana ilikuwa ni siku ya kuzaliwa ya Ambwene Yesaya aka AY ambapo ametimiza umri wa miaka 30.
East Africa Radio walimtembelea nyumbani kwake ambapo alikuwa amealika washkaji na ndugu kula bata za hatari.
Kuna mengi ya kuvutia aliyoyaongea lakini moja wapo ni kuwa meneja wake Hemdee Kiwanuka ambaye tarehe 27 mwezi huu atamdondosha Jason Derulo nchini Rwanda kwenye fainali za mashindano ya muziki ya Primus Guma Guma, amemsurprise kwa kumwambia kuwa Jason angependa ampongeze kwa party ya nguvu japo siku yake ya kuzaliwa imepita (5,July).

Ay amesema Jason aliyetamba na ngoma kama ‘Whatchu Say’ na ‘What if’ amesikiliza nyimbo zake japo hawajaongea chochote kama wanaweza kufanya collabo ama lah!
Baada ya Jason kusikiliza ngoma hizo na kupewa historia fupi ya AY na meneja wake,Jason akasema itakuwa poa akimwandalia pia party yake ya kizushi mzee wa commercial!
Amesema mwezi huu utakuwa ni mwezi wa kula bata zaidi kwakuwa pamoja na kuandaliwa party nchini Rwanda, Kiwanuka amesema atamwangushia party nyingine jijini Nairobi.
Hopefully, akikutana na Jason Derulo, uhakika wa kufanya collabo ni mkubwa.