Pages

Saturday, September 15, 2012

GHARAMA YA MAKOMEDIANI NI BANGI, GONGO NA,,,,!!

Crispin Masele
Masele moja kati ya Makomediani wakongwe Swahiliwood.
UTAFITI unaonyesha kuwa pamoja wasanii wa komedi yaani wachekeshaji kuwa ni wasanii wasiokuwa na makuu katika maisha yao, lakini utata umetanda katika malipo yao na maisha yao kwa ujumla, hivi karibuni kuna mjadala umezuka katika vyombo vya habari vikielezea gharama za komedi hizo kuwa chini katika utayarishaji.

Crispin Masele
Masele akiwa katika pozi.
FC imebaini kuwa baadhi ya watayarishaji wanavyotaka kuandaa filamu uandaa bajeti ya lakini mbili tu kwa ajili ya malipo ya wasanii hiyo ni kwa mtayarishaji asiye mchekeshaji wala hayupo karibu na wasanii wa Komedi lakini kwa mchekeshaji kama ataamua kuandaa filamu lazima basi anaweza kuandaa kuwaandalia washiriki Bangi, Gongo na ugali mkubwa.
Kwa mchekeshaji matata kidogo anaweza kununulia Bia na kuanza kurekodi komedi husika, jambo ambalo baadhi ya wachekeshaji wamekiri kutokea kwa jambo hilo huku wakidai kuwa baadhi ya wachekeshaji hawajitambui jambo ambalo limefanya waandaaji kuwatumia kwa gharama ndogo huku wakifanya kazi kubwa.
.
Onyango Bashir
Onyango, akiwa na Bashir wakiwa wamekaa na wasanii wengine.
Hussein Mkiety
Sharomilionea
Lucas Mhuvile
Joti mchekeshaji anayetoka katika kundi linaloongoza kwa malipo Orijino Komedi.
Wakati gharama za filamu hata mbovu uchukue kiasi cha milioni mbili na na kwenda juu zaidi hali haipo hivyo katika Komedi, malipo ya msanii mmoja ambaye hana jina ambayo ulipwa kwa kushiriki filamu kama malipo utumika kutengenezea Komedi hadi kukamilika kwa ajili ya kuingia sokoni.
Msanii pekee ambaye analipwa malipo makubwa tofauti na wasanii wengine ni Amri Athuman ‘King Majuto’ akifuatiwa na Salum Haji ‘Mboto’ na Mboto ameweza kulipwa malipo hayo kutokana na utengenezaji wake kuwa ni tofauti kwani anawashirikisha wasanii wa filamu na si wachekeshaji.
Thamani ya komedi imeshuka sana katika malipo na hata wasanii, lakini jambo ambalo wanatakiwa kujifunza ni kutoka kwa wasanii wenzao wa Orijno Komedi ambao wameweza kujijengea utaratibu kuwa na kiwango kikubwa cha malipo huku wakiweza kuwa na msimamo katika kulinda maslahi yao.
Iwapo kama Komedi imerekodiwa na kukamilika kwa gharama ya laki sita kwa kila kitu je Wasanii kama Senga, Dani na wengine walioshiriki wamelipwa shilingi ngapi? Mpiga picha kalipwa shilingi ngapi? Mhariri naye je? Uigizaji ni kazi kama zilivyo kazi nyingine kama msanii atakuwa hajalipwa vema sanaa itaendelea kweli?
.
Sarafina Kidole
Sarafina akiwa na mchekeshaji mwenzake.
Kama ni kweli malipo ya kazi zenu ni Gongo, Bangi na Ugali mkubwa kwa ngulu tafuteni staili nyingine ili maisha yaende hivi karibu Mzee king Majuto alisema bora aachane na uigizaji hasa wa Komedi kwa sababu wachekeshaji wanafanya utani yeye anauza Komedi moja kwa milioni nane kumbe kuna komedi za lakini sita na zina nyota wengi!
Wasanii wa Komedi wanatakiwa kumshukru sana mkurugenzi wa Al Riyamy Production ambaye kwanza amebadilisha mfumo wa komedi na kuweza angalaukushindana na filamu japo si sana, siku za nyuma watayarishaji wa Komedi walikuwa hawana bajeti wa mavazi lakini kwa sasa si haba, Hongera Halfan Abdalah.