Saturday, June 23, 2012

GODZILLA - NATAKA

Mwaka huu msanii wa hip hop nchini, Godzilla ameamua kuja na mtindo mpya wa kuachia nyimbo.
Msanii huyo ambaye wakati mwingine unapomsikiliza unaweza ukahisi unamsikiliza 50 Cent, ametoa video yake mpya iitwayo ‘Hard Work Pays.’
Pia ataachia wimbo kwenye radio uitwao ‘Nataka’ huku nyimbo zote hizo zikiwa zimefanywa na producer Marco Chali.

Godzilla alisema ametoa video ya hard work pays ili kuzungumzia jinsi ambavyo anauchukulia usupastaa kama zawadi ambayo wasanii wanatakiwa kuiheshimu.
Anasema kwa namna ambavyo wasanii wanapata mafanikio kutokana na muziki hawana budi kumkumbuka mwenyezi Mungu na kuendelea kuwa na heshima.

Aliongeza kuwa wimbo huo ameutoa ili uwe kama somo kwa wasanii na watu wengine.
Godzilla alisema ameamua kutoa video na wimbo kwa wakati mmoja kwakuwa amegundua kuwa nyimbo za hip hop anazozitoa zimekuwa zikichezwa kwenye vipindi vya radio vya aina moja, huku vipindi vya asubuhi na muda mwingine vikishindwa kuzicheza.
Hivyo anaachia ‘Nataka’ ulio katika mtindo tofauti ili uweze kuwepo kwenye rotation ya vipindi vyote vya radio.