Showing posts with label audio. Show all posts
Showing posts with label audio. Show all posts

Thursday, August 23, 2012

New Song: BEN POL - PETE

My new song PETE  is my first single after the Maboma album which I did with MLab.  Thank God it's been a great journey and I personally feel the singles of that album were great. I have now come with a new production team and heading for my second album. Share it and I hope you enjoy this record as much as I enjoyed recording it. Peace and much love.

Song Detalis:
     Artist: Ben Pol
     Song: Pete
     Songwriters: Fred Max, Ben Pol & Lady Peace Winnie
     Producer: Mona Gangsta
     Studio: Classic Sound
     Genre: R&B/Soul
     Year: 2012

Ben Pol-Pete lyrics
Verse 1;
Hadithi ya penzi langu umenikata nini mwisho
huthamini huoni pendo lako nalihitaji leo kesho
 nishawahi kukosa ,mwenzenu nilisumbuka
 mchana na usiku mimi, nishawahi kukosa
nasema niliteseka mchana na usiku mimi
nishawahi kukosa ,mwenzenu nilisumbuka
 mchana na usiku mimi, sitaki tena kosa
najua nitateseka
mwisho sitokuwa nawe tena naulizaa

Chorus;
Kama pete yangu, inakuchomaa kidoleni
ni kama pendo langu , linakuchoma moyonii ,
bora kuitoa aaah aah ,
pendo kulivua aaah ,
bora kuitoa ,
moyoni mwangu mi nisiteseke
bora kuitoa aaah aa ,
pendo kulivua aaah ,
bora kuitoa ,
moyoni mwangu mi nisiteseke

Verse 2;
 sikujali wambea wanafki walosema
hatutadumu mimi nawe tutajaachana
wakiniona siko nawe si ndo watasema
hata nyumbani watajua tumefarakana
nikiwaza kwenda mbali ,moyoni nahofia
maana bado nakujali ,kwako nilishatua
nikiwaza kwenda mbali ,moyoni nahofia
maana bado nakujali ,kwako nilishatua
kila jema n'tendalo mie ,kwako limekuwa sio
nitakapo kujua ulipo ,wanijibu utakavyo
pete kidoleni mwako ,yanisuta mwenzio
ndo maana nikukosapo ,moyo wanienda mbio

Repeat Chorus till fade

Sunday, August 12, 2012

NEW HIT: TIP TOP CONNECTION - RIZIKI


                       DOWNLOAD  "TiPtOp CONECTION - Riziki (Prods By Maneck).mp3"

NEW HIT: BAGHDAD FT AMIN - NIMEWASAMEHE


Track ; nimewasamehe

Artist  ; Baghdad ft  Amini

Studio ; Shine rec

Producer ; Mr t 

Project ; wajukuuu int

   Hii  ni ngoma iliyojko katika muendelezo wa project za msanii ambae awali alikuwa akiunda kundi la Mexicana lacavela ambao ndio wanaotazamiwa kuwa mahasimu wake wakubwa kwa kipindi hichi chote tangu Baghdad alipotangaza kujitoa Mexicana lacavela mwishoni mwa mwaka jana. Baghdad ; mimi nilikuwa kama pm (program manager ) na manager wangu wa sasa alikuwa kama manager baada ya meesen kuachia ngazi  na ndipo tuliamua kupanga mikakati ili kuipeperusha bendera ya Mexicana ila haikufanikiwa kwa kuwa baadhi ya wasanii waliokuwa wakiunda kundi hilo kuhisi wamefika safari yao. Baghdad aliamua kujitoa na kuamua kufanya project zake kama solo artist chini ya manager wa zamani wa mexaicana lacavela anaefahamika kama daudi lucas kwenye jina lililopo kwenye id yake. Hivyo maisha mengi aliyopitia aliamua kuyaweka kwenye wimbo wake mpya aliouachia tar 11 mwezi 1gust 2012  mwezi ambao amezaliwa mama yake mzazi, kaka yake, na manager wake ameuita mwezi wenye Baraka kwake na upendo ndio maana ameamaua kukaa both na kutunga nyimbo kwa ajili ya kuwasamnehe wote waliowahi kumkosea, Baghdad ; unajua aidea alinipa manager wangu ilikuwa ni chungu cha pili wakati tunafuturu akaniambia si vyema kufunga wakati una dukuduku moyoni  so wasamehe watu waliokukosea na ndipo niliamua kukaa na kutunga ngoma iliowasamehe wale waliowahi kunitishia kuniua, walionichukulia mademu wangu kipindi nasoma, walionisingizia mambo nisiyofanya, niliowalaza hom wakati wamefukuzwa kwao na hawana pakwenda nikawa nawapa chakula, kwa zaidi ya miezi mitatu, kunao wengine walionikera kipindi nafanya kazi clouds media group, na zaidi ni mtu ambae nimemsaidia kufanya studio yake ijulikane tangu inaanza mpaka hapa ilipofika ila akadiriki kumtaka msichana ambae na diriki kusema ni furaha yangu ya milele aitwae anitha. Nimeamua kuwasamehe wote. Wote kama kuna yeyote aliyewahi kunikosea iwe kwa kutenda, kwa kufanya, kwa kuwaza au kwa njia yoyote nimemsamehe. Aidha baghda ameeleza ya kuwa kwa sasa hana majibizano yeyote na mtu yeyote kwa sababu kashasahau yote yaliowahi kutokea kitambo now nawaza jinsi ya kukabiliana na wasanii wa kimataifa ambao natarajia kufanya kazi nao.  

"baghdad ft amin - nimewasamehe.mp3"

Sunday, August 5, 2012

new hit: WATANASHATI - WATASUBIRI

Ngoma Mpya Ya Kundi zima la Mtanashati all starz linaloundwa na Dogo Janja , Suma Mnazareti, Pnc ,Amazon na Happy Balyce Chini ya Uongozi wa Ostazi Juma na Musoma .. Ngoma inaitwa WATASUBIRI na imetengenezwa na Mesen Selkta chini ya DE FATALITY music
 DOWNLOAD:  "Watanashati+(+Suma+Mnazaret+,+Dogo+Janja,+Amazon,+PNC,+Happy+Balyce+)+-+Watasubiri.mp3"

Saturday, August 4, 2012

UCHAMBUZI WA NGOMA YA Izzo B Ft. Belle 9 – Utarudishwa




Wiki hii Izzo B ameachia ngoma yake mpya iitwayo Utarudishwa, aliyomshirikisha Belle 9. Ngoma imefanywa na maproducer wawili. Beat imetengenezwa na the rapper turned producer One the Incredible na baadaye Izzo akaenda hadi Morogoro kwenye studio za Dirty Mode Records ambako producer Tris alimalizia kazi iliyosalia. Panel ya TMP inauchanachana wimbo huo kama ifuatavyo:

Josefly

Kwanza kabisa niseme tu nilikua surprised kidogo niliposikia beat ya hii ngoma ameinyonga One the incredible, big up kwake kwa kuwa multi talented, japo naona inaendana na ile ya IZZO B ft. Suma lee, IZZO BUSINESS ,au hizi ndo beat za IZZO B.! Ila ni beat nzuri ya Hip Hop.
Sasa nazama deep kwenye ngoma yenyewe na nitaegemea kwenye mashairi na utunzi wa hii ngoma, kwa ufupi tu hii ngoma nina mengi ya kuielezea kwa kuichalenge na kuisifia pia ila nitayafupisha. Naanza na challenge ili zieleweke mapema.

Wimbo ni wa kawaida, kama mtu anamjua Izzo B, sio mbaya na wala siwezi kusema ni wimbo mkali, labda tu niseme wimbo ni mzuri, hapo naamini nimeeleweka, sio mkali ila sio mbaya pia.

Huu ni wimbo wa hip hop ambao umeandikwa kama ‘free of style’, kwa wafuatiliaji wa hip hop watakua wamenielewa zaidi ya ile maana ya freestyle iliyozoeleka. Kiitikio cha wimbo kinaashiria tu kumuonya Izzo kwa anachokisema kuwa kinaweza kupelekea yeye kurudishwa kwao Mbeya. Na hapo ndo hiyo free of style inanifanya nisikilize ili nijue kasema nini Izzo hadi his big boy Belle anamtahadharisha kua atarudishwa kwao Mbeya baada tu ya verse ya kwanza, nilijua atasema chochote coz chorus haimbani ila nahisi itakua ni mambo fulani mazito hata kama ni majigambo.

Daah, bahati mbaya kiukweli Izzo hakuweza kwa asilimia 100 kunipa kile nilichotegemea, japo sijui angeimba nini kwa sababu the song is free of style kwa hiyo nitahukumu nilichosikia tu, mi naona kwa hii chorus nadhani ameitendea haki kwa asilimia 70 hivi kiuandishi, ni asilimia kubwa labda ndo sababu wengi hawatashitukia, ila sikiliza tena na tena na nifatilie ninachosema pia. Verse ya kwanza aliianza vizuri ila mi naona kabisa ikiingia chorus labda neno analomaliza nalo ndo linaipa push kidogo chorus kuanza hivo. Ila duh..bado kidogo.

Chorus ya maneno mawili naona kama imezidi kidogo uzito kile kilichoimbwa, jaribu kusikiliza kwa makini jinsi Belle 9 anavyomtahadharisha, tengeneza picha ya hii tahadhari na mashairi anayoingia nayo Izzo B, ni majigambo ya kawaida tu ambayo yangekaa kwenye chorus yoyote ya majigambo, haya maneno mawili ya kwenye chorus ni ya kawaida sana ila yanatoa picha nzito saaana ya kinachoimbwa so mashairi ya Izzo kama kidogo yamezidiwa uzito kwa mtazamo wangu. Na hapa napapigia mstari.

Pia kuna mstari naona kama Izzo aliamua tu kumtaja Chidi, “natubu kama Chid japo sitokei Ilala” kweli kuna uhusiano kati ya kutubu na Chidi kwa ngoma yake ya NATUBU..lakini mi sioni mahusiano yanayoleta maana kati ya kutubu na kutokea Ilala. Inamaana wanaotubu sana ni wa Ilala? Najua imezoeleka sana kutumia aina hii ya uandishi ila hapa pande mbili hazina mahusiano, hasa kutubu na kutokea ilala, imejazilisha tu line!

Mbali na hayo, kiukweli sijasikia tofauti sana kati ya hii ngoma ya Utarudishwa na Ile Izzo Business, chukua hizi ngoma mbili zisikilize then utaona ni kama kapita njia moja ila kabadili tu mavazi, ni mulemule kwa msemo wa kisasa. Mashairi yamebadilika kidogo, lakini hii ni kama part 2 hivi kwa maudhui, na nadhani haya mashairi pia yanakaa kwenye ile chorus ya IZZO BUSINESS aliyofanya Suma Lee zaidi ya huku kwenye hii chorus ya Belle 9 kimaudhui.

Tukiachana na hizo changamoto, Izzo B amebarikiwa kughani kwa ladha fulani nzuri kusikiliza katika kila neno analotamka kwa Kiswahili au kiingereza, pia kuna maneno mazuri na punch line au ‘mistari konde’ mingi kwenye hii ngoma, na maneno yanayojenga picha flani nzuri sana.
Mashairi kama mashairi tu yako poa. Stile ya kuwakilisha mashairi iko poa na imeendana na beat. Ni hayo tu.

Kinye

Karibu Izzo kwenye uwanja wetu.

Utarudishwa Mbeya”…nadhani ingekuwa hivyo, si kwa ubaya lakini ni kama haijitoshelezi kuitwa utarudishwa, ni kama kinywa kinadai maneno zaidi kuridhika.

“One”…mkali wa michano ambaye haoni future yake kutakata nje ya muziki (nilibahatika kumsikia akijinadi hivyo siku moja). Mdundo huu umenifanya nianze kuamini kuwa akijitahidi basi kweli ndoto yake ya kuwa bonge la mundaaji yaweza timia kwani huu umekuwa mwanzo mzuri huku nikiwa naamini kuwa kitaalamu anahitaji mawili matatu kuweza kuimarika zaidi.

“Belle”…BLOG hii imemtunuku taji la ukali wa chorus kitu ambacho kilikuwa kigumu kupinga kwakuwa ni kweli tupu. Nimefurahi hajakomaa kama anavyokomalia viitikio vingine, hii imetoa ladha mpya na tamu japo mpaka sasa natamani sauti ya Izzo isingekuwa inasikika kwenye kiitikio ili kuleta maana zaidi!! Kwa maoni yangu angeachwa Belle kuamua namna ya kukamilisha maneno yote ya chorus kwa namna yake.

“Izzo”…toleo lako lingine hili ambalo si baya kiukweli japo pia si zuri kupita matoleo yako yote mengine. Siku zote nimekuwa nikipenda mawazo yako ya kiuandishi na mtindo wako ambao kwa kiasi una upekee…hongera kwa hili.
“Tris ”…bado sina mengi juu yako kwakuwa wafanya vizuri japo si kupita wote, pokea hizo pongezi. Kwenye wimbo huu na nyingine zoote kila neno litamkwalo naamini haki yake ni kusikika kwa ufasaha, kama hili tunakubaliana basi niseme ulipitiwa kidogo kuruhusu sisi kutosikia baadhi ya maneno kwenye wimbo huu, nazungumzia kwenye kiitikio ambapo kuna maneno sijayasikia yanatamkwa kumaanisha nini, na shida imekuja baada ya wewe “kubend pitch” ya maneno hayo…kiukweli mimi sikuona umuhimu wake pale.
Amani Joakim

Ni Ngoma nzuri sana,nafikiri hakuna muziki mbaya hata siku moja.. Hata Hivyo, nimemskia Izzo B akiimba nyimbo kama hii zaidi ya mara tatu,sidhani mimi kama mskizaji ningependa kusikia kitu hicho hicho hata kama ni kizuri kutoka kwa mtu mmoja.

Ana uwezo wa kubadilika na nina hakika ana vitu vingine lakini akifuta ile formula ya "FOLLOW THE SUCCESS TREND UNTILL IT BREAKS" nafikiri inaweza kumfikisha pabaya. Ukifuata hii formula unaeeza ukakuta mashabiki wako baadhi wanakufuta kwenye list zao halafu kurudi itakugharimu nguvu kama vile unaanza Muziki.

Belle 9 kama kawaida amefanya vizuri kwenye sauti za Chorus. Kwenye swala la Mdundo..Ni Beat nzuri sana hasa ikiwa imetengenezwa na mtu aliezoeleka kama Artist. Mdundo una hadhi zote za hip hop.
Nafikiri mdundo huo una purpose ya watu kusikiza kinachosemwa zaidi hivyo mtu halisi aliyetakiwa kukaa ni yule mwenye maneno ya msingi lakini yasiyochosha pia..kama ONe The Incredible Vile..

Asilimia 90 ya wasanii Bongo na hata America wanahitaji beat nzito na yenye vionjo vingi ili kuweka mzani pale ambapo mashairi yake yanapokua dhaifu kidogo,ndio maana ni mara chache utamskia ama usimskie kabisa Nas/common kwa beats za Timbaland ama Polow Da Don ama Jim Jonsin (wote wamefanya nao lakini sio watu wao wa mara zote) ni kutokana uzito wa mashairi yao unaitaji kitu simple kama Mdundo huu, ambacho producers hao ambao ni Heavy Hitters sio mikato yao.

Ushauri wangu ni kwamba Izzo afanye mpango wa kubadili hii formula ya Political Theme ambayo ameifanya mara kadhaa tayari kabla haijamuharibia.
Lakini pia inaweza kuwa ni formula inayomfanya awe Izzo B. Kwa kuwa yeye ni msomi nafikiri atafanya utafiti kabla ya kuchukua hatua yoyote ya mabadiliko. Pia awe mwangalifu na aina ya midundo anayochagua mingine ni hatari kwa afya ya career yake. N:B. Mawazo haya ni ya kwangu binafsi, nina haki ya kueleza na sio shuruti kuyafuata.

J-Ryder

Kwa Beat Making, One Incredible amejitahidi, compared na kipinde cha nyuma, back then.

Sample ingekaa poa ingeongezwa Stereo Widening, ipo sana Mono.
Kwa Chorus, sijapenda pale Belle 9 anaposema "Izzo, izzo", kama wange umiza kichwa zaidi, ila kipande cha pili "utarudishwa Mbeya" naona imekaa sawa.

Upande wa vocals, ukisikiliza vizuri unaweza hisi kuwa imekuwa recorded pembeni tu ya computer equipments, na kama ni kwenye booth ama vocal room, basi Acoustic Treatment yake bado sio nzuri.

Kwenye Bass, ingewekwa Bass Amps ili kuongeza Volume yake...na pia ku-separate Bass na Kick by cutting unwanted frequencies.

Bila shaka ngoma imekaa okay, mixing tu hapa na pale, automations kidogo..itakaa sawa.
thanx http://leotainment.blogspot.com/

Friday, August 3, 2012

SIKILIZA INTERVIEW YA KWANZA YA HERMY B KUHUSU SHAVU LA UNIVERSAL MUSIC GROUP

                    Hermy B With Universal Music Group Executive Director....Mr. Lindelani

Hermes Tyrol Lyimo (Hermes Hermy B)             
     Kutokana na maombi ya wadau wengi Music kuomba kupata ufafanuzi zaidi jinsi Producer  HERMY B ni vipi alipata shavu kubwa kama ili lakujiunga na Universal Music Group.


Timu nzima ya

The JUMP OFF

Times Fm TZ  


iliongea na Hermy B na hiki ndicho alichosema

 

new single DOGO JANJA ft PNC - YA MOYONI


Ngoma  Mpya ya Dogo janja amemshirikisha Pnc wote wakitokea basement ya Ostazi Juma Na Musoma . Ngoma inaitwa Ya Moyoni nma Ngoma imepikwa Mj records na MARCO cHALI .

Friday, July 20, 2012

Rick Ross ft Jay-Z & Dr. Dre – 3 Kings

 Rick Ross releases the most anticipated record off his “God Forgives, I Dont”! ’3 Kings’ features Jay-Z and Dr. Dre and is produced by Jake One! Album in stores July 31st!


Download:      "Rick Ross ft Jay-Z & Dr. Dre - 3 Kings.mp3"

Sunday, July 15, 2012

Soulja Boy Feat. Jazz Lazer – On That Ho ( 2o12 )

 

                            NEW Extremely HOOOOOOOOOOOT Tracks to : "Soulja Boy
 DOWNLOAD:  "Soulja Boy Feat. Jazz Lazer - On That Ho ( 2o12 )www.dj-ku.blogspot.com.mp3"

NEW SONG BY SMILE - NICHEKECHE

Hey Guyz.......tnx kwa supt ya wimbo wake wa kwanza KICHEFUCHEFU Hii ni single ya pili imefanyika Sharobaro Rec
We nid ur supt once again....tnxxxxxxxxxxxx
Kwa chochote kuhusu smile hii ni 4n number yake 0656132708

                                       DOWNLOAD ; "Smile - Nichekeche.mp3"

D’banj releases hot new single, ‘Oyato’

  



Produced by: J Sleek
Source: DBANJRECORDS

I think D'banj is doing real music for the first time. The musical exposure his is getting is making him put out something nice. Oyato is a nice song for me. At least for once, I can relate to what a Nigerian Artiste says blended in fine Afro tunes. This is how our Nigerian music should be showcased to the world. Well done D'banj.

What is Oyato? Oyato simply means different or unique in the Yoruba language - from Nigeria (it also happens to be my name backwards with an “o” at the end).

DOWNLOAD "dbanj - oyato.mp3"