Mrs. Okoye
Mrs. Okoye amekuwa akiumwa kwa mrefu ugonjwa ambao bado
haujajulikana.
Pamoja na Peter na Paul, watoto wake wengine Jude na Ajeh
wana mchango mkubwa kwenye muziki wa Nigeria.
Peter na Paul enzi za utoto |
Wakati kila mtu anajiuliza nini chanzo cha kifo cha mama
yao, mtandao wa niyitabiti.net umebaini kuwa baada ya kuanza kuumwa alipelekwa
kwenye hospitali ya St. Nicholas Hospital, miongoni mwa hospitali ghali zaidi
nchini Nigeria.
Baadaye alipelekwa nchi za nje kwa matibabu zaidi. Bahati
mbaya amefariki wakati akiendelea na matibabu hayo.
Muda mfupi baada ya habari hiyo kujulikana, marafiki na
jamaa walianza kutuma salamu za rambirambi kwa familia ya Psquare.
Katika maisha yake, mama huyo anafahamika kwa mchango mkubwa
kwa mafanikio ya watoto wake.
Leo hii P-square ndo wanamuziki wanaolipwa pesa nyingi zaidi
nchini Nigeria na barani Afrika kwa ujumla.