Monday, July 9, 2012

UWOYA ANAHITAJI MAOMBI


LAANA? Irene Pancras Uwoya si yule, amebadilika na hivi karibuni aliwaacha midomo wazi wakazi wa mkoani Tanga baada ya kumwaga ‘mitusi’ mizito hadharani, Ijumaa Wikienda lina kisa kamili.
Mtiti huo ulijiri hivi karibuni kwenye Baa ya Nyinda jijini humo ambapo Uwoya alikuwa mmoja wa wahudhuriaji wa tamasha la wazi la filamu, Tanzania Open Film Festival lililofanyika katika Viwanja vya Tangamano.
Shushushu wetu alimshuhudia mwanamama huyo akijitwika ulabu ndipo akatokeza paparazi mmoja aliyetaka kumtandika picha, ndipo pakachimbika.
“Unaambiwa Uwoya alinyanyuka na chupa akitaka kumtandika paparazi huyo huku akishusha mvua ya matusi lakini kabla ya kumrushia chupa wasanii JB (Jacob Steven), Ray (Vincent Kigosi) na Richie (Singo Mtambalike) ikabidi wafanye kazi ya ziada kutuliza hali ya hewa,” alisema shuhuda wetu.
Katika tukio hilo watu wengi walimshuhudia akifanya tukio hilo hivyo kumtoa kwenye ule usemi kuwa msanii ni kioo cha jamii.
Ijumaa Wikienda lilipomtafuta kujua kama alifanya vile kwa sababu ya ulevi au alikuwa akimaanisha, kwa bahati mbaya simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa.
 ijumaawikienda11