Showing posts with label bongo. Show all posts
Showing posts with label bongo. Show all posts
Wednesday, December 11, 2013
Friday, November 29, 2013
Hermy B afunguka kuhusu uhusiano kati yake na AY na FA
Hermy B afunguka kuhusu uhusiano kati yake na AY na FA,asema kazi zinakuja
Moja kati ya habari nzuri ambazo zimewasurprise watu wengi leo ni kuhusu kurudi kwa urafiki uliokuwa umevunjika kati ya Hermy B, AY na mwana FA. AY na FA wamempa kampani kubwa producer Hermy B kwenye birthday party yake iliyofanyika usiku wa kuamkia leo na kupost picha kwenye mitandao ya kijamii.Tovuti ya Times Fm imefanya mahojiano na Hermy B ambaye tayari ameingia nchini Kenya kwa ajili ya kuendelea na majukumu yake ya ujaji kwenye shindano Tusker Project Fame huku akisherehekea siku yake ya kuzaliwa leo (November 29).
Akiongelea kuhusu uhusiano uliopo kati yake na maswahiba wawili kwenye muziki AY na FA ambao awali walitofautiana kikazi na kila mmoja kuendelea kivyake, Hermy B amesema yeye na wasanii hao walimaliza tofauti zao siku nyingi na wamekuwa wakiishi kama washkaji kwa muda mrefu japokuwa hawakuweka kwenye media.
“By the way mimi na AY na Mwana FA unajua tunakutana mara nyingi sana, yaani tunapokutana ni nje ya nyumbani kwangu ambapo utanikuta niko mimi, AY, Mwana FA, yupo Fid Q, Salama unamkuta yuko pale. So, most of the time tuko pamoja, hii ni kitu tu tumewaonesha kwamba as much as watu walikuwa wanafikiria labda kuna kitu kinaendelea lakini hapana, sisi tuko peace long time tumeamua ku-reveal tu sasa hivi,”
“Kiukweli sisi ni washikaji ambao tuko tight sana, nafikiri jamii tu ndio inaelewa kivingine. Unajua watu wengi wanafikiri mkishindwa kuelewana kitu fulani basi hamuwezi kuelewana, hapana…kwa sababu imagine sisi kila siku jioni kabla sijaingia kwenye nyumba yangu kulala nakutana na AY tunakaa tunapiga story mpaka saa nane za usiku ndo kila mtu anaenda kwake kulala,” amefunguka Hermy B.
Amesema hivi karibuni alikuwa na AY Nairobi, na walikaa na Fid Q na Prezzo na kupiga story usiku wote hadi asubuhi.
Hermy ambaye ni producer na C.E.O wa B’Hits amezungumzia mpango wao wa kufanya kazi tena kama ilivyokuwa zamani.
“Kazi tutafanya, unajua hizi ni plans za mbeleni na tumekuwa tunaongea ni jinsi gani tunaweza tukafanya kazi vizuri na kwa faida zaidi na kila mtu awe na furaha moyoni mwake unajua. Kwa hiyo kazi zitakuja hatuwezi kuwaambia lini, kesho kutwa au mwezi ujao.”
Ladha ya ngoma kali zitakazopikwa tena kama ‘Habari Ndio Hiyo’ itawakusanya tena mashabiki wa B’Hits, AY na FA pamoja kwa ajili kuusapoti muziki mzuri. Lini hasa?
Ameeleza Hermy B, “time ikifika, the right time statement itatoka kwamba tunafanya nini pamoja au nini kinaendelea interm of kazi and then wale mashabiki wote ambao walikuwa wanatupenda watatujoin watuongezee nguvu sasa tuweze kuifikisha Tanzania ambapo inatakiwa ifike.”
Monday, November 25, 2013
WANITAMANI NDIO UJIO MPYA WA BELLE 9
Belle 9 kuachia wimbo mpya kesho, unaitwa 'Wanitamani', asema ameufanya kiafrika zaidi
Belle 9 toka Morogoro ambaye ni moja kati ya vocalists bora Tanzania ataachia ngoma mpya kesho (November 26), ngoma aliyoipa jina la ‘Wanitaka.’
Akiongea na DJ K U, Belle 9 amesema mdundo wa ngoma hiyo umefanywa na Producer wake aliyemtoa ‘Tris’ ambae hivi sasa yuko Afrika kusini kimasomo na kwamba vocal amefanya kwa producer Mona Gangster.
Akiongea na DJ K U, Mkali huyo wa ‘Listen Now’ amesema ngoma hiyo iko katika mahadhi ya kiafrika na inayochezeka na pia imebeba ujumbe wa mapenzi.
“Hiyo ngoma ni muziki flani hivi wa kiafrika kwa sababu sasa hivi African Music ndio muziki ambao umeiteka dunia nzima hata wasanii wa Afrika wanauza sana huko Ulaya. Watu wamezoea kunisikia sana kwenye beat za R&B sana, kwa hiyo round hii nimechange kidogo ili kutengeneza mazingira ya hata kupata nafasi sehemu za mbali.” Amefunguka Belle 9.
Alieleza pia kuhusu ujumbe alioujaza kwenye ‘Unanitaka’, “Ngoma inaelezea wanawake ambao wana-fake kwa sababu kwenye hali ya kawaida wasanii huwa tunasumbuliwa sana kwamba I love You, I love You, lakini ni kwa sababu tu we ni star.”
Sunday, November 24, 2013
ANGALIA PICHA ZA KWENYE SHOW YA P-SQUARE TISHA SANAAAAAA
Peter na Paul Okoye wa kundi la P-Square wakilivamia jukwaa la Leaders usiku huu.
Mashabiki wakipagawa na shoo ya P-Square.
Joh Makini akilitawala jukwaa.
Nikki wa Pili (kushoto) na G Nako wakifanya yao stejini.
Kundi la Weusi likiongozwa na Joh Makini likishambulia jukwaa la Leaders Club
kabla P-Square
hawajapanda usiku huu.
waliohudhuria shoo ya P-Square Live in Dar ndani ya Viwanja vya Leaders
Club
vilivyopo Kinondoni jijini Dar.
Nyomi baada ya kuikubali vilivyo shoo ya Profesa Jay.
Mwanamuziki
Judith Wambura 'Lady Jaydee' au 'Anaconda'
akiwapagawisha mashabiki
wake waliohudhuria katika Viwanja vya Leaders Club
usiku huu katika shoo
wa wakali P-Square.
Watu... Jideeeeeeeeeeee...
Machozi Band nao walikuwepo kumback up Jide.
Mwanamuziki Ben Pol akiwasha moto katika steji ndani ya Viwanja vya Leaders
usiku huu katika shoo ya P-Square Live in Dar.
Nyomi ikifuatilia shoo ya Ben Pol.
Ben Pol akiimba sambamba na mwanadada.
picha kutoka GlobalPublishers
Friday, November 22, 2013
B'Hits yatoa ufafanuzi kuhusu kuwaondoa Mabeste, Vanessa na Gosby
Jana B’Hitz Music Group iliweka wazi uamuzi wa kuwaondoa kwenye label hiyo wasanii watatu ambao ni Vanessa Mdee, Mabeste na Gosby.
Japokuwa Vanessa na Mabeste walitangaza wiki hii kujitoa kwenye label hiyo, huku Gosby akiwa bado hajasema chochote, timu ya BHits imesema kuwa wasanii hao waliondolewa kwenye label hiyo miezi miwili iliyopita japokuwa hawaamua kutangaza.
Mabeste aliiambia Times fm kuwa ameamua kujiondoa katika label hiyo kwa kuwa muziki wake ulikuwa haumlipi na kwamba maisha aliyokuwa anaishi ndiyo yaliyopelekea yeye kudhaniwa kuwa anafanya show za nje, na kwamba amechoka kuwa mzigo kwao.
Tovuti ya Times fm ilimtafuta Amani Joachim ambaye ni mwana sheria na Chief Operations Officer wa B’Hits Music Group ili kufahamu kuhusu sababu alizozitoa Mabeste kwa upande wa B’Hits, na mikataba ikoje na kama watachukua hatua zozote za kisheria.
“Hiyo statement ambayo Mabeste ameamua kuisema kwangu mimi naona haiko sawa kabisa. Sisi ni ndugu na tulikuwa tunaishi hivyo, tatizo la mtu mmoja ni tatizo la mtu mwingine yaani tunakuwa pamoja kabisa. Na kuna vitu vingi ambavyo Mabeste anajua kwamba tunavifumbia macho. Hata hiyo mikataba, sisi na Mabeste kuna kipindi tume-deal hata bila mikataba na mambo yakawa safi tu kwa sababu kuna ile heshima na kuaminiana.” Amesema Amani.
Ameyaelezea pia madai ya Mabeste kuwa mabadiliko yake katika maisha ndiyo yaliyosababisha B’Hits kuhisi kwamba anapiga shows za nje.
“Mabeste inabidi aangalie statements zake, na muda ambao anaamua kutoa hizo kauli kwa sababu kati yetu sisi tuna siri nyingi sana (Mabeste na Upande wa B’Hits). Tusifike sehemu kwamba tukaanza kufaidisha kila mtu, hicho ndicho kitu ambacho ningependa kukiweka sawa. Hizo shows na vitu vingine ambavyo labda alikuwa anavifanya akiwa nje tunavifahamu vingi tu, lakini kutokana na ule u-brother na nini tunavichunia tu.” Ameeleza kiongozi huyo wa B Hits.
Hata hivyo Amani amekubaliana na kuwepo kwa ubovu wa soko la muziki ambapo amesema hata shows zikiwepo bado malipo yanayotolewa yako chini kiasi kwamba Kampuni haliwezi kuendeshwa kwa kutegemea kugawana kipato hicho na msanii.
Aliongelea pia madai ya Mabeste kuwa B’Hits haikuwa inamfanya atengeneze pesa kupitia muziki wake.
“Well, hopefully kule anakoenda atapata. Tunaelewa Mabeste ana majukumu, maisha yake tunajua kwamba yamebadilika kwa namna flani. Personally nafahamu, sijui akina Harmy na Pancho. That’s why I’m ready to stay quiet kwenye vitu kama hivyo, nilikuwa tayari kukaa kimya…sina haja ya kufunguka ni vitu vingapi ambavyo Mabeste ameshafanyiwa katika hali ya u-brother, I will not say them kwa sababu kipindi mimi navifanya nilivifanya katika good will na nilitaka iishie hivyo, Amani will never say them.”
Jana C.E.O B Hits Hermy B aliuambia mtandao wa Bongo5 kuwa Vanessa, Gosby na Mabeste hawana shukurani kwa kile ambacho B Hits imewafanyia na kutoa mfano kuwa alitoa shilingi million nane mfukoni kulipia video ya Closer ya Vanessa na kiasi kingine kulipia kazi alizofanya nje ya studio za B Hits, fedha ambazo hazijawahi kurudi.
Nae Amani Joachim alitoa ushauri kwa Vanessa, Mabeste na Gosby kwa ujumla kuwa wawe na amani na waendelee kufanya mambo yao na kuacha kutengeneza vita kati yao na B’Hits kupitia media kwa kuwa hata yeye ameamua kuyafumbia macho mengi.
Lakini vipi kuhusu hasara ambayo B’Hits itaipata kutokana na kuondoka kwa wasanii hao kwa kuwa walichukuliwa wakiwa hawana majina na wakati huu wanaondoka wakati wameanza kuwa productive.
Mwana sheria na Chief Operations Officer wa B’Hits anaeleza.
“They were real productive na naweza kukwambia kweli hawa watu wako very talented, na B’Hits haijawahi kum-house mtu ambaye ni mbovu, na ndo maana watu wanashangaa kwa nini mna nyumba kubwa ya media halafu mna watu watatu tu, sisi kuna kipindi tulikuwa na msanii mmoja tu Mabeste for like 4 years, ni kwa sababu tunaangalia talent.
“Na kusema kwamba sasa hivi tutakuwa hatujarudi nyuma utakuwa ni uongo, kuondoka kwao ndio tutarudi nyuma steps kadhaa, lakini pia kutokana kwamba plans tulizopanga kufanya wakati tukiwa nao zilikuwa hazijafika kuiva, we are ready to do that with someone else, Mungu hajagawa kipaji kwa watu wawili au watatu.”
Amesema anaamini baada ya Gosby, Vanessa, na Mabeste watakuja watu wengine ambao wana vipaji pia.
Kauli ambayo inaungana na ile ya Hermy B kuwa B’Hits itatangaza wasanii wapya wa label hiyo mwanzoni mwa mwaka ujao.
Tovuti ya Times fm ilitaka kufahamu kutoka kwa mwana sheria huyo kuhusu mkataba kati ya B’Hitz na wasanii hao na damages/athari za kuvunja mkataba huo zikoje na iwapo watawadai wasanii hao.
Amesema mikataba ilikuwa tight lakini kwa mazingira ya Tanzania na hali halisi ya kipato cha wasanii wa Tanzania hiyo mikataba inakuwa kama useless kwa kuwa kiasi kinachotakiwa kulipwa na msanii huyo ni kikubwa kuliko hali halisi ya maisha ya msanii husika.
“Ukimchukua bwana mti ukampeleka mahakamani, mahakama inaangalia damage ambayo imeingia katika kampuni, na mwisho wa siku inachukua maamuzi ambapo itakwambia bwana mti kama amepatikana na kosa amlipe bwana jose million 150 Kwa mfano, haimfungi. Problem ni kwamba bwana mti hana hata shilling 200 mfukoni mwake, we unadhani utamfanyaje bwana mti?” Alieleza kwa mfano.
“Kwa sababu mahakama ikishakupa judgement inakuacha ukatafute hiyo hela, haimfungi mtu. Kesi za madai sio kesi za jinai..sasa hapo imagine hapo ni wasanii wangapi leo unawafanyia kazi ya million 40 Million 50, ambayo ukiingia katika intellectual property court (mahakama ya maswala ya copy right), na copy right ni very expensive, tunaongelea six figures, eight figures. Sasa angalia ni wasanii wangapi hapa Tanzania wanaweza kukulipa eight figures.?” Amesema.
Kutokana na hali hiyo amesisitiza kuwa kuna haja ya kuwalipa wasanii pesa nyingi katika kazi zao huko wanakoenda kufanya ili wanapopata matatizo waweze kulipa, na kwamba bila hivyo mikataba ya label na wasanii Tanzania itakuwa useless.
Hii inamaanisha kuwa hakuna hatua zozote za kisheria ambazo B’hits itachukua kudai fidia kutoka kwa wasanii hao.
Hata hivyo uongozi wa B’Hits umesema utaachia nyimbo nyingine za wasanii hao zilizoko studio na kwamba zitachezwa redioni, lakini wasanii hao hawatakuwa na haki ya kuzitumia kwa kuwa ni mali halali ya kampuni hiyo.
Wednesday, November 13, 2013
Promoter DMK aeleza kwa nini wasanii wa hip hop Bongo hawapati shows Marekani kama waimbaji, awashauri cha kufanya
Promoter DMK, mtanzania anayefanya kazi ya kuwapeleka
wasanii wa Afrika nchini Marekani na kuwaleta wamarekani Afrika, amesema
wasanii wa bongo wanaofanya hip hop wanapata changamoto zaidi ya nafasi
ya kupiga shows Marekani kwa sababu ya lugha wanayotumia na kwamba kule
kuna watu wengi wanaofanya hip hop halisi.
DMK ambaye pia anamiliki kituo cha radio na TV ‘Swahili radio&TV’ kilichoko Marekani, amefunguka katika kipindi cha ‘The Jump Off’ cha 100.5 Times fm alipokuwa akipiga story na Jabir Saleh, Dj D_Ommy na Dj K_U kuhusu fursa za wasanii wa bongo kupiga shows Marekani kupitia kampuni yake ya ‘DMK Global’.
“We unakuja unaimba hip hop halafu unaimba Kiswahili, ujue inakuwa kazi kidogo kwa sababu kule watu wanaimba hip hop na wanafanya ile yenyewe, sasa wewe unakuja unaimba Kiswahili inakuwa inasumbua kidogo.” Alisema DMK.
Promoter huyo aliwashauri wasanii wa Hip Hop kitu cha kufanya ambacho kitawawezesha kupiga shows Marekani na kukubalika pia.
“Sisi tunajaribu kidogo kuwaambia hawa wanamuziki wa hapa wapige muziki ambao uko commercial kidogo, kwa sababu muziki ni business sasa kama muziki ni business inabidi wacommercialize muziki wao.” Alisema DMK.

Friday, May 10, 2013
Unakumbuka Raha za ki-legendary za muziki?
Unakumbuka? Raha za ki-legendary za muziki wa Silent Inn, Bills, FM Club, Carlifonia Dreamers, Mambo Club,na Tazara? Basi DJ John Dillinga (DJ JD) na DJ Fast Eddy tunawakaribisha kujumuika na malegends wenzako kila jumamosi kuenzi nyakati hizo Isumba Lounge, Jolly Club kwa mchango wa elfu 10 tu mlangoni, Karibu Sana.
Friday, November 2, 2012
The LEGEND IS BACK LADIES NIGHT
This Saturday at synergy lounge jds
entertainment presents the legend is back ladies night ladies night
excursion ,ladies come in a group of five and receive a very treat all
the way from the entry to the club,plus some serious good music from
yours trully JOHN DILLINGA (DJ JD) along side his long time dj friend dj
FAST EDDY ,guys you all know what to do ,JOIN THEM LADIES .entry
10000 sh only you are all welcome
Friday, September 21, 2012
Tuesday, September 18, 2012
DITTO ANAOMBA KURA ZETU WATANZANIA KWENYE TUZO ZA DISCOVERIES 2012.
Nyota wa kizazi kipya anayejulikana kwa jina la Lameck Ditto kutoka hapa
bongo land Tanzania amechanguliwa katika kuwania tuzo za Radio France
International Discoveries
ambazo zitakuwa zinatolewa nchini France.katika tuzo hizi wasanii kumi
kutoka Africa wamechanguliwa katika kuwania tuzo hizi na Ditto naye ni
moja kati ya wasanii ambao wametajwa katika list ya wasanii ambao
watashiriki katika kuwania tuzo za Radio France Intenational
Discoveries.Kama mshindi akipatikana katika tuzo hizo za Radio France
International basi atajipatia Euro elfu kumi na mkataba wa kufanya
show live katika nchi 18 Duniani.Kwa hiyo tuna mtakia ushindi katika
tuzo hizi za Radio France International
Bonyeza hapa chini kuingia kwenye site ya kumpigia kura
Saturday, September 15, 2012
GHARAMA YA MAKOMEDIANI NI BANGI, GONGO NA,,,,!!
UTAFITI unaonyesha kuwa pamoja wasanii wa komedi yaani wachekeshaji
kuwa ni wasanii wasiokuwa na makuu katika maisha yao, lakini utata
umetanda katika malipo yao na maisha yao kwa ujumla, hivi karibuni kuna
mjadala umezuka katika vyombo vya habari vikielezea gharama za komedi
hizo kuwa chini katika utayarishaji.
FC imebaini kuwa baadhi ya watayarishaji wanavyotaka kuandaa filamu uandaa bajeti ya lakini mbili tu kwa ajili ya malipo ya wasanii hiyo ni kwa mtayarishaji asiye mchekeshaji wala hayupo karibu na wasanii wa Komedi lakini kwa mchekeshaji kama ataamua kuandaa filamu lazima basi anaweza kuandaa kuwaandalia washiriki Bangi, Gongo na ugali mkubwa.
Kwa mchekeshaji matata kidogo anaweza kununulia Bia na kuanza kurekodi komedi husika, jambo ambalo baadhi ya wachekeshaji wamekiri kutokea kwa jambo hilo huku wakidai kuwa baadhi ya wachekeshaji hawajitambui jambo ambalo limefanya waandaaji kuwatumia kwa gharama ndogo huku wakifanya kazi kubwa.
.
Wakati gharama za filamu hata mbovu uchukue kiasi cha milioni mbili na na kwenda juu zaidi hali haipo hivyo katika Komedi, malipo ya msanii mmoja ambaye hana jina ambayo ulipwa kwa kushiriki filamu kama malipo utumika kutengenezea Komedi hadi kukamilika kwa ajili ya kuingia sokoni.
Msanii pekee ambaye analipwa malipo makubwa tofauti na wasanii wengine ni Amri Athuman ‘King Majuto’ akifuatiwa na Salum Haji ‘Mboto’ na Mboto ameweza kulipwa malipo hayo kutokana na utengenezaji wake kuwa ni tofauti kwani anawashirikisha wasanii wa filamu na si wachekeshaji.
Thamani ya komedi imeshuka sana katika malipo na hata wasanii, lakini jambo ambalo wanatakiwa kujifunza ni kutoka kwa wasanii wenzao wa Orijno Komedi ambao wameweza kujijengea utaratibu kuwa na kiwango kikubwa cha malipo huku wakiweza kuwa na msimamo katika kulinda maslahi yao.
Iwapo kama Komedi imerekodiwa na kukamilika kwa gharama ya laki sita kwa kila kitu je Wasanii kama Senga, Dani na wengine walioshiriki wamelipwa shilingi ngapi? Mpiga picha kalipwa shilingi ngapi? Mhariri naye je? Uigizaji ni kazi kama zilivyo kazi nyingine kama msanii atakuwa hajalipwa vema sanaa itaendelea kweli?
.
Kama ni kweli malipo ya kazi zenu ni Gongo, Bangi na Ugali mkubwa kwa ngulu tafuteni staili nyingine ili maisha yaende hivi karibu Mzee king Majuto alisema bora aachane na uigizaji hasa wa Komedi kwa sababu wachekeshaji wanafanya utani yeye anauza Komedi moja kwa milioni nane kumbe kuna komedi za lakini sita na zina nyota wengi!
Wasanii wa Komedi wanatakiwa kumshukru sana mkurugenzi wa Al Riyamy Production ambaye kwanza amebadilisha mfumo wa komedi na kuweza angalaukushindana na filamu japo si sana, siku za nyuma watayarishaji wa Komedi walikuwa hawana bajeti wa mavazi lakini kwa sasa si haba, Hongera Halfan Abdalah.

Friday, August 24, 2012
Subscribe to:
Posts (Atom)