Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, imejipanga kuazisha wodi za kisasa
za kulipia 'Fast track', katika Hospitali ya Mwananyamala ambazo
zitatoa huduma bora kwa wananchi.
Naibu Meya wa Manispaa hiyo,
Bw. Songoro Mnyonge, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akitoa
ufafanuzi juu ya hatua walizo zichukuwa kuhakikisha wananchi wanapata
huduma bora za matibabu katika hospitali hiyo, “Tunaamini mwaka huu wa
fedha, tutaanzisha huduma hii katika Hospitali ya Mwananyamala, ingawa
watalipia lakini mgonjwa atajisikia faraja zaidi kupata huduma bora kwa
gharama ndogo, hadi sasa tuna wataalamu wa kutosha,” alisema.
Alisema
kwa kuanzia, watakuwa na wodi ya wanawake, wanaume na wataanza kuchukua
wagonjwa ambao ni wanachama wa Bima za Afya na baadae wanatarajia kuwa
na wodi ya watoto, “Tumeamua kuanzisha huduma ya matibabu ya kulipia kwa
sababu baadhi ya Watanzania hawana utamaduni wa kwenda kutibiwa katika
hospitali za umma,” alisema.
Alitoa wito kwa wananchi kuwa na
tabia ya kwenda kuhudumiwa katika hospitali za umma ambazo zina usalama
mkubwa kwa afya zao na wataalamu wazuri.
Darlin Said