Friday, June 29, 2012

MADEE: NIPO TAYARI KUMSAIDIA DOGO JANJA

Baada ya Dogo Janja kuondoka na kwenda Arusha mpaka anarudishwa Dar na kundi la Watanashati Madee hakutaka kuzungumza chochote kuhusu madai yaliyotolewa na Dogo Janja kwamba hakulipwa hela ya album hata pesa ya showz zenyewe account yake haikuwahi kufikisha kuwa na milioni moja bank.

Amesema “unajua watu hizi habari wamezipokea tofauti labda kwa sababu ya Dogo Janja alikwenda kwenye Media kuongea vitu ambavyo sikudhani kama atakuja kuviongea kwa sababu ni maisha ya ndani ya familia, lakini yule mimi ni mwanangu.. mtoto akikunyea mkononi unaambiwa nenda kanawe, huwezi kuukata mkono wako kwa hiyo siku yoyote time yoyote mi namkaribisha Dogo Janja atakapojisikia kufanya kazi na Tip Top au Madee mi niko tayari kwa sababu sidhani kama anaweza kusema hawezi kufanya kazi na Madee kwa sababu asilimia 100 ya kazi zake ambazo watu wanazisikia zimetokea kwa Madee kwa hiyo bado anahitaji mchango mkubwa sana kutoka kwangu”
“kikubwa ambacho namshauri sana kama karudi Dar es salaam azingatie elimu, muziki upo tu atakuja kufanya muda wowote.. kikubwa ugomvi wake ulikua ni shule tu lakini hivyo vingine ambavyo vimeongeleka, vimeongeleka tu haviwezi kuzuilika na mtu yeyote hata mimi siwezi kuvisikia, nimemsamehe… muda wowote anapotaka msaada kutoka kwangu niko tayari”