Wednesday, June 27, 2012

Mwana Fa featuring AY n Dully Sykes - Ameeen (Lyrics)


Ni MwanaFA
Yupo na Dully Sykes
Silent Ocean
Inna Mi Yard
Keeping The Good Music Alive
Yessayah
Choras:
Ameen/Ameen Ameen/Mungu niongezee/
Ameen/Ameen Ameen/
Nishike mkono niongozee *2

Verse 1..
Ziende,on and on kama Eryka Badu/wafahamu sababu/ni heshima kwa Mungu/natembea kifua mbele yote sababu ya wewe/wote wanaojipindua mwisho wanasanda wenyewe/binamu yangu Masumbuko ananisikia hata akiwa jela/jinsi nakinukisha na bado juhudi na sala/naomba hekima za Suleiman/sio miguvu ya bure/hata kauli zangu ndogo zionyeshe nilienda shule/maadui wafunge mikono nimewazidi wape ishara/wape akili za hasara wachezee kazi na mshahara/ikidunda sana inakaribia kupasuka/yangu ikeshe isiishe leo hata wajukuu wanaikuta/bora kuchekwa kuliko kuchekwa sana wanaonipinga waumize,Mungu nakomba sana/uwape umri mrefu wa kwangu na wa babu yangu/ili roho zao ziumie wakiona mabalaa yangu/Amen..

Choras:
Ameen/Ameen Ameen/Mungu niongezee/
Ameen/Ameen Ameen/
Nishike mkono niongozee *2

Verse 2..
Nisichokijua hakiwezi kunisumbua/wakisema mabaya yashindwe kunifikia/wape kismati cha paka cha kupendwa na wachawi/mi naomba cha pesa na kwa ujinga niwe kiziwi/wape wanawake wazee na mafukara halafu wagonjwa/ama mabwana mabwabwa wasiogonga kabla ya kugongwa/wanaomba nisiwe na kitu ili niombe waninyanyase/dhiki inijae vyote vya kwangu wavipate/kuna viumbe hata huwajui na bado wana beef na wewe/kama wanichukue msukule nisionekane wabaki wenyewe/naishi kwa kudra,baraka,matakwa yako/siwezi nikachemsha kama ukibaki upande nilipo/competition is irrelevant/with you by my side/nafanya siongei na wanajua mi ni mastermind/haraka zaidi yao/uchungu zaidi yao/ukubwa au udogo wa tatizo unaletwa na akili zao/it's a wrap

Choras:
Ameen/Ameen Ameen/Mungu niongezee/
Ameen/Ameen Ameen/
Nishike mkono niongozee

Bridge:
Mi nna haraka zaidi yao/pia hata uchungu zaidi/rhumba,likinipiga,nazidi kukugeukia kwako Muweza/zaidi yao/pia hata uchungu zaidi/rhumba,likinipiga,nazidi kukugeukia kwako Muweza/