Friday, May 10, 2013

SPOKEN NIGHT

Unakumbuka Raha za ki-legendary za muziki?

Unakumbuka? Raha za ki-legendary za muziki wa Silent Inn, Bills, FM Club, Carlifonia Dreamers, Mambo Club,na Tazara? Basi DJ John Dillinga (DJ JD) na DJ Fast Eddy tunawakaribisha kujumuika na malegends wenzako kila jumamosi kuenzi nyakati hizo Isumba Lounge, Jolly Club kwa mchango wa elfu 10 tu mlangoni, Karibu Sana.

Friday, November 2, 2012

The LEGEND IS BACK LADIES NIGHT

This Saturday at synergy lounge jds entertainment presents the legend is back ladies night ladies night excursion ,ladies come in a group of five and receive a very treat all the way from the entry to the club,plus some serious good music from yours trully JOHN DILLINGA (DJ JD) along side his long time dj friend dj FAST EDDY ,guys you all know what to do ,JOIN THEM LADIES .entry 10000 sh only you are all welcome

Tuesday, September 18, 2012

DITTO ANAOMBA KURA ZETU WATANZANIA KWENYE TUZO ZA DISCOVERIES 2012.


Nyota wa kizazi kipya anayejulikana kwa jina la Lameck Ditto kutoka hapa bongo land Tanzania amechanguliwa katika kuwania tuzo za Radio France International Discoveries ambazo zitakuwa zinatolewa nchini France.katika tuzo hizi wasanii kumi kutoka Africa wamechanguliwa katika kuwania tuzo hizi na Ditto naye ni moja kati ya wasanii ambao wametajwa katika list ya wasanii ambao watashiriki katika kuwania tuzo za Radio France Intenational Discoveries.Kama mshindi akipatikana katika tuzo hizo za Radio France International basi atajipatia Euro elfu kumi na mkataba  wa kufanya  show live katika nchi 18 Duniani.Kwa hiyo tuna mtakia ushindi katika tuzo hizi za Radio France International
Bonyeza hapa chini kuingia kwenye site ya kumpigia kura

Saturday, September 15, 2012

GHARAMA YA MAKOMEDIANI NI BANGI, GONGO NA,,,,!!

Crispin Masele
Masele moja kati ya Makomediani wakongwe Swahiliwood.
UTAFITI unaonyesha kuwa pamoja wasanii wa komedi yaani wachekeshaji kuwa ni wasanii wasiokuwa na makuu katika maisha yao, lakini utata umetanda katika malipo yao na maisha yao kwa ujumla, hivi karibuni kuna mjadala umezuka katika vyombo vya habari vikielezea gharama za komedi hizo kuwa chini katika utayarishaji.

Crispin Masele
Masele akiwa katika pozi.
FC imebaini kuwa baadhi ya watayarishaji wanavyotaka kuandaa filamu uandaa bajeti ya lakini mbili tu kwa ajili ya malipo ya wasanii hiyo ni kwa mtayarishaji asiye mchekeshaji wala hayupo karibu na wasanii wa Komedi lakini kwa mchekeshaji kama ataamua kuandaa filamu lazima basi anaweza kuandaa kuwaandalia washiriki Bangi, Gongo na ugali mkubwa.
Kwa mchekeshaji matata kidogo anaweza kununulia Bia na kuanza kurekodi komedi husika, jambo ambalo baadhi ya wachekeshaji wamekiri kutokea kwa jambo hilo huku wakidai kuwa baadhi ya wachekeshaji hawajitambui jambo ambalo limefanya waandaaji kuwatumia kwa gharama ndogo huku wakifanya kazi kubwa.
.
Onyango Bashir
Onyango, akiwa na Bashir wakiwa wamekaa na wasanii wengine.
Hussein Mkiety
Sharomilionea
Lucas Mhuvile
Joti mchekeshaji anayetoka katika kundi linaloongoza kwa malipo Orijino Komedi.
Wakati gharama za filamu hata mbovu uchukue kiasi cha milioni mbili na na kwenda juu zaidi hali haipo hivyo katika Komedi, malipo ya msanii mmoja ambaye hana jina ambayo ulipwa kwa kushiriki filamu kama malipo utumika kutengenezea Komedi hadi kukamilika kwa ajili ya kuingia sokoni.
Msanii pekee ambaye analipwa malipo makubwa tofauti na wasanii wengine ni Amri Athuman ‘King Majuto’ akifuatiwa na Salum Haji ‘Mboto’ na Mboto ameweza kulipwa malipo hayo kutokana na utengenezaji wake kuwa ni tofauti kwani anawashirikisha wasanii wa filamu na si wachekeshaji.
Thamani ya komedi imeshuka sana katika malipo na hata wasanii, lakini jambo ambalo wanatakiwa kujifunza ni kutoka kwa wasanii wenzao wa Orijno Komedi ambao wameweza kujijengea utaratibu kuwa na kiwango kikubwa cha malipo huku wakiweza kuwa na msimamo katika kulinda maslahi yao.
Iwapo kama Komedi imerekodiwa na kukamilika kwa gharama ya laki sita kwa kila kitu je Wasanii kama Senga, Dani na wengine walioshiriki wamelipwa shilingi ngapi? Mpiga picha kalipwa shilingi ngapi? Mhariri naye je? Uigizaji ni kazi kama zilivyo kazi nyingine kama msanii atakuwa hajalipwa vema sanaa itaendelea kweli?
.
Sarafina Kidole
Sarafina akiwa na mchekeshaji mwenzake.
Kama ni kweli malipo ya kazi zenu ni Gongo, Bangi na Ugali mkubwa kwa ngulu tafuteni staili nyingine ili maisha yaende hivi karibu Mzee king Majuto alisema bora aachane na uigizaji hasa wa Komedi kwa sababu wachekeshaji wanafanya utani yeye anauza Komedi moja kwa milioni nane kumbe kuna komedi za lakini sita na zina nyota wengi!
Wasanii wa Komedi wanatakiwa kumshukru sana mkurugenzi wa Al Riyamy Production ambaye kwanza amebadilisha mfumo wa komedi na kuweza angalaukushindana na filamu japo si sana, siku za nyuma watayarishaji wa Komedi walikuwa hawana bajeti wa mavazi lakini kwa sasa si haba, Hongera Halfan Abdalah.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...