Belle 9 kuachia wimbo mpya kesho, unaitwa 'Wanitamani', asema ameufanya kiafrika zaidi
Belle 9 toka Morogoro ambaye ni moja kati ya vocalists bora Tanzania ataachia ngoma mpya kesho (November 26), ngoma aliyoipa jina la ‘Wanitaka.’
Akiongea na DJ K U, Belle 9 amesema mdundo wa ngoma hiyo umefanywa na Producer wake aliyemtoa ‘Tris’ ambae hivi sasa yuko Afrika kusini kimasomo na kwamba vocal amefanya kwa producer Mona Gangster.
Akiongea na DJ K U, Mkali huyo wa ‘Listen Now’ amesema ngoma hiyo iko katika mahadhi ya kiafrika na inayochezeka na pia imebeba ujumbe wa mapenzi.
“Hiyo ngoma ni muziki flani hivi wa kiafrika kwa sababu sasa hivi African Music ndio muziki ambao umeiteka dunia nzima hata wasanii wa Afrika wanauza sana huko Ulaya. Watu wamezoea kunisikia sana kwenye beat za R&B sana, kwa hiyo round hii nimechange kidogo ili kutengeneza mazingira ya hata kupata nafasi sehemu za mbali.” Amefunguka Belle 9.
Alieleza pia kuhusu ujumbe alioujaza kwenye ‘Unanitaka’, “Ngoma inaelezea wanawake ambao wana-fake kwa sababu kwenye hali ya kawaida wasanii huwa tunasumbuliwa sana kwamba I love You, I love You, lakini ni kwa sababu tu we ni star.”