Thursday, June 14, 2012

WAJUA SABABU YA DOGO JANJA KUFUKUZWA TIP TOP CONNECTION?



            Sababu zilizotajwa na Tip Top Connection ni kwamba Dogo Janja alilewa sifa na kuwa mtoro shuleni.
 Sababu toka kwa DOGO janja ni uonevu na dhuluma ndivyo vilivyomchosha kuishi Dar es Salaam.

Anasema tangu aje Dar es Salaam hajawahi kusaidiwa chochote na Madee zaidi ya mambo ya muziki pekee huku kula, malazi na ada ya shule vikifanywa na rafiki yake Madee aitwaye Abdallah Doka ambaye (Dogo Janja) alikuwa akiishi kwake.

 Anasema kutokana na ngoma zake kujipatia umaarufu alikuwa akipata show nyingi nchini na zote alikuwa halipwi chini ya milioni moja. Kilichokuwa kinamsikitisha anasema ni kulipwa hela kidogo isiyozidi laki mbili na hivyo kumfanya aishi kwa tabu licha ya kuingiza hela nyingi za show.
 “Nilikuwa navumilia tu kwasababu kila nilipolalamika kuhusu mambo ya hela Madee alikuwa mkali sana,” ameongea uchungu.
Dogo Janja anasema ilikuwa inafikia wakati akifanya show za ukumbuni hulipwa elfu hamsini au chini ya hapo na wakati mwingine alikuwa halipwi kabisa.
Tamaa ilizidi kumwingia Madee kiasi cha kumnyang’anya kadi yake ya benki na kuanza kuchukua hela bila kujua password aliipata wapi.
“Kuna wakati nilikuwa nataka kumtumia mama laki moja, Madee akanikataza eti kwakuwa watadhani nina hela sana,”

 
Dogo Janja anaeleza kuwa inamuuma sana kwakuwa muziki haujampa chochote licha ya Madee ambaye huwa hapati hata show kumtumia kimaslahi na hadi leo hii anamalizia kujenga nyumba yake.

              “Ni kama vile Madee alinipanda ili anivune.”

 Ameendelea kusema kuwa hiyo juzi sasa hadi kufikia Tip Top watangaze kumfukuza alikuwa kwa Tundaman akipiga story na Madee akamuita kisha kuanza kumpiga.

 Alichukua simu yake akaondoka nayo. “Jamaa alianza kujitumia meseji kutoka kwenye simu yangu kwenda kwake za matusi ama kuwa nataka kumroga.

          Nimebahatika kusoma hizo meseji zakutoka ktk simu ya DOGO JANJA kwenda kwa mama yake kuwa amechoka mateso ya Mlezi wake na anataka kurudi ARUSHA na meseji nyingine ilikuwa na maneno makali.

    JANJA amesema Kitendo cha kumwambia Madee kuwa amechoka na anataka kurudi nyumbani ndicho kimemfanya amfanyie yote hayo hadi kumwambia kuwa watahakikisha wanambania asifanye vizuri tena kwenye muziki. Pia amedai kuwa Madee aliwapigia simu wazazi wake ili wamkataze Dogo Janja asifanye interview na vyombo vya habari.