Thursday, June 21, 2012

WOLPER AFUNGUKA SKENDO YA KUNYANG'ANYWA GARI

http://api.ning.com/files/R2ijbELhVHjBe864gprHTJBt7R4JxL8*zt4wTlV1vihhyYuFcuM5noYa7QTnMotOx7eCDzQLeEp0s-5W2Ut3kAKeA8lzkGaR/bmwyawolper1.jpg
Shakoor Jongo na Musa Mateja
TETESI zimezagaa jijini Dar es Salaam kuwa staa wa sinema Bongo, Jacqueline Wolper Masawe amenyang’anywa lile gari lake aina ya BMW X6, lenye namba za usajili T 574 BXF na kwamba, sasa nyota huyo anatembelea gari lake la zamani Toyota Noah, Amani limeshibishwa taarifa.
Chanzo cha kuenea kwa tetesi hizo kilianzia kwenye mitandao ya kijamii, hasa blog na BBM ambapo wadau waliandika kuwa Wolper alinyang’anywa gari hilo na mwanaume aliyemnunulia.
Aidha, wadau wengine walikwenda mbele zaidi wakitaja jina la Frank ambaye ni mtoto wa mfanyabiashara maarufu jijini Dar kuwa ndiye mmiliki wa gari hilo kwa sasa.
Baada ya kupata taarifa hizo, Jumatatu wiki hii, saa saba mchana timu ya Amani iliingia mzigoni kusaka ukweli wa taarifa hizo ambapo mtu wa kwanza kuzungumza naye alikuwa Wolper mwenyewe ambaye alikiri kusikia taarifa hizo huku akikanusha kuwa si za kweli.
“Na mimi nimesikia lakini si kweli jamani. Hivi mtu anaweza kunyang’anywa nguo yake ya ndani au shati lake? Si itakuwa kichekesho, gari ni mali yangu na hakuna mwenye uwezo wa kuja kuninyang’anya kwani nalimiliki kihalali,” alisema Wolper.
Aidha, staa huyo mwenye kuandamwa na matukio kwa siku za karibuni, alisema amelifungia gari hilo nyumbani kwake, Mbezi Beach, Dar kwa sababu lina matatizo kidogo.
Amani halikukubaliana na utetezi wake, likamtaka Wolper kuongozana na mapaparazi wake ili kwenda Mbezi kuliona gari hilo kama lipo kweli au kulifikisha ofisi za Global.
Wolper: “Nisikuongopee kuwa naweza kuja nalo hapo ofisini wakati tatizo lake nalifahamu mimi, nakuja kuwachukua twendeni nyumbani mkalione.”
Saa 2:16 usiku, Wolper aliongozana na mapaparazi wetu hadi nyumbani kwake na kulikuta gari hilo likiwa ndani ya geti.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, staa huyo alilionesha gari hilo huku akimwaga machozi na kusema:
“Watu wananionea sana, wananichafua. Sijui lengo lao ni nini hasa? Kila kukicha nasingiziwa jambo, mara Jack kafanya hivi, mara vile.
“Mbaya zaidi, hata waigizaji wenzangu wapo wanaonichukia, au kwa kuwa nimepata maendeleo kidogo? Walitaka niporomoke kimaisha?”
Licha ya kupata uhakika kuwa Wolper hajanyang’anywa gari hilo, pia alionesha kadi yake ya umiliki.

 http://www.globalpublishers.info/