Friday, July 6, 2012

Hermy B: Sijawahi kuitumia degree yangu


Producer na mwenyekiti mtendaji wa B’Hits Music Group Ltd, Hermes Tarimo aka Hermy B amesema katika maisha yake hajawahi kuitumia degree aliyoihangaikia kwa miaka mitatu chuo kikuu.
Hermy B ambaye alifahamika kama producer wa muziki kupitia kazi alizowafanyia MwanaFA na AY amesema hayo katika mahojiano na website ya Tusker Project Fame ambapo yeye ni jaji wa mashindano hayo.
Producer huyo amesema chuoni alisoma masomo ya sayansi ya wanyama na degree kubaki kwenye kabati tu bila kuitumia kwa kazi.
Alisema alipokuwa chuoni alikuwa akitumia muda mwingi kutengeneza beat kitu ambacho kiliwafanya wazazi wake kugombana mara kwa mara. Baba yake alimtaka mwanae kuzingatia masomo zaidi wakati mama yake alikuwa akimpa moyo kufuata kile moyo wake unataka ilimradi tu asifeli masomo.
Aliongeza kuwa familia yao iliishi nchini Marekani kwa miaka mitano alipokuwa mtoto mdogo na baba yake alikuwa shabiki wa Hip hop. Na ndo maana alisema hiyo iliathiri nyimbo anazotengeneza kwakuwa nyingi ni za hip hop, japo ameshatengeneza nyimbo zenye mahadhi ya Afro fusion na Bongo Flava.
Hermy B alieleza kuwa pamoja na uprodusa yeye pia ni mwanamuziki na ameshatengeneza albam tatu. Hata hivyo ni wimbo mmoja tu ndo umewahi kusikika na ulifanya vizuri. Licha ya hivyo amesema haamini kama ana sauti nzuri ya kuimba ndo maana amejikita katikia production zaidi. Alisema yuko mbioni kuachia albam yake ya tatu iitwayo Read Autotune.
Mambo mengine usiyoyajua kuhusu Hermy B
- Hulala kwa karibu masaa 10 kwa siku
- Hajawahi kutengeneza beat kwenye studio,hutengeneza kwenye laptop yake
- Muziki kwake ni part time business