Thursday, July 19, 2012

ORIJINO KOMEDI WAMTOSA MASANJA


Masanja Mkandamizaji.


MEMBA wenzake msanii wa Kundi la Orijino Komedi, Masanja, akina Joti wamemtosa mwenzao huyo kwenye uzinduzi wa albamu yake ya nyimbo za Injili.
Kwa mujibu wa chanzo, Jumapili iliyopita, Masanja aliambatana na wasanii kibao wa Bongo Movie mjini Iringa kwenye kuzindua albamu yake hiyo ya nyimbo za dini lakini bila wasanii wenzake.
“Yaani huku nawaona mastaa kibao wa Bongo Movie, lakini wasanii wenzake Masanja, akina Joti hakuna hata mmoja,” kilisema chanzo hicho.
Jitihada za kuwapata wasanii hao hazikuzaa matunda kwani simu zao hazikupatikana hewani.