Friday, July 27, 2012

SHEHE AZIFUMUA SWAUMU ZA MASTAA



Jacqueline Wolper.

Flora Mvungi.

Aunt Ezekiel.
Rose Ndauka.
Na Hamida Hassan
SHEHE Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salum amezifumua swaumu za baadhi ya mastaa ambao hufunga bila kufuata taratibu za dini ya Kiislam.
Akizungumza na Ijumaa katika mahojiano maalum, Shehe huyo alisema funga ina taratibu zake hivyo mastaa wanaoingia kwenye ibada hiyo bila kuzifuata ni sawa na kushinda na njaa.
Alisema kitendo cha mastaa kufunga kisha baada ya kufungua kuendelea kufanya mambo yaliyo kinyume na Uislam ni sawa na kuoga kisha kuingia kwenye tope.
“Itakuwa ni jambo la ajabu kama utakuwa umefunga kisha kuendelea kuvaa vimini, kunywa pombe, kuzini au usiku unakwenda klabu. Wanaofanya hivyo ndani ya mwezi huu, ni sawa na kusema hawajafunga,” alisema shehe huyo.
Aidha, amewashauri mastaa Aunt Ezekiel, Jacqueline Wolper, Rose Ndauka na Flora Mvungi ambao katika siku za hivi karibuni walitangaza kusilimu kutobadilisha maamuzi yao kwani kufanya hivyo itakuwa ni kumcheza shere Mungu.
“Kwa hawa waliobadili nawasihi wasirudi nyuma na hata wakifunga wafuate maandiko yanasemaje, wasipofanya hivyo mwisho wao unaweza kuwa motoni,” alisema Shehe Musa.