Friday, July 6, 2012

USIKU WA MATUMAINI NI KESHO UWANJA WA TAIFA

Bondia Francis Cheka (katikati) akitamba mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuwa atamchakaza mpinzani wake Japhet Kaseba.
Wolper (kulia) akijitapa kuwa atamtwanga mpinzani wake mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani).
 
Kocha wa Wema, Rashid Matumla (wa tatu kushoto) akizungumza kwa niaba ya Wema (ambaye hakuwepo) kwenye mkutano huo.
Nahodha wa Bongo Fleva, H Baba (kulia) akiahidi ushindi kwa timu yake dhidi ya Bongo Movie.
Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na (kutoka kushoto) kocha wa bondia Francis Cheka (Abdalah Saleh Komando), Francis Cheka, meneja wa mfuko wa elimu (Charles Kapima), mmoja wa waratibu wa tamasha hilo (Luqman Maloto), promota wa pambano hilo, Kaike Silaju, bondia Japhet Kaseba na mwisho ni meneja wa Kaseba (Idd Bakari).
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.
WAKATI homa ya mapambano ya ndondi yanayosubiriwa kwa hamu kati ya Francis Cheka na Japhet Kaseba pamoja na wakali wa filamu nchini, Wema Sepetu na Jacqueline Wolper, ikizidi kupanda, baadhi ya mabondia hao wametoa tambo kuwa watawachakaza wapinzani wao siku hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari asubuhi ya leo kwenye hoteli ya kisasa ya The Atriums jijini Dar, Jacqueline Wolper alitamba kumpiga vibaya mpinzani wake siku ya Jumamosi kwenye Tamasha la Matumaini pale Uwanja wa Taifa.
“Sipendi maneno, napenda vitendo, nimekuwa nikisikia Wema na rafiki yake wanaongea sana kuhusu mimi kwenye TV.
“Nataka nikate mdomo wake siku hiyo kwa kumpiga" alisema Wolper. Nae Bondia Francis Cheka alitamba kuwa kama kawaida yake atamchachafya mpinzani wake katika tamasha hilo.