Tuesday, July 10, 2012

Wakamatwa Wakisafirisha Bangi kwenye Madumu Ya Mafuta Ya Kula-Iringa

Hawa ni askari Polisi wa Mjini Iringa, usidhani walikuwa wakinunua mafuta ya kula, Hapana. Ndani ya madumu hayo ya kuhifadhia mafuta walibaini kuwepo kwa bangi iliyokuwa ikisafirishwa kupelekwa Tunduma, Mbeya
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Peter Kakamba akitoa na kuonesha bangi kutoka katika moja ya madumu ya mafuta aina ya Oki.
Fadhil Juma (kushoto) na Baraka Mwinuka (kulia) wakiwa ndani ya ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa baada ya kukamatwa na kilo 60 za bangi zilizokuwa zimejazwa ndani ya madumu ya mafuta ya kula yaliyotobolewa kwa chini