Friday, August 10, 2012

ASKARI ALIYEWALIPUA WENZAKE MOROGORO ADAIWA KUJINYONGA


Mwili wa marehemu Donald Mathew ‘Dunga’ ukining'inia mtini..
Wananchi wakishuhudia mwili wa ‘Dunga’ .Mwili wa Donald Mathew ‘Dunga’ ukiondolewa mtini.
Mwili wa Donald Julius ukibebwa kupelekwa kwenye gari la polisi.
...Ukiingizwa kwenye gari la polisi.
Barua ya Dunga kwa Waziri wa Mambo ya Ndani.
ASKARI jasiri aliyejizolea sifa mkoani hapa kwa kitendo chake cha kuwataja hadharani baadhi ya askari wenzake akiwashutumu kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za kushirikiana na majambazi kufanya uharifu, Donald Julius Mathew,  mwenye namba ya jeshi la polisi F3276 amekufa akidaiwa kujinyonga.                
Mwili ya afande huyo ambaye ni maarufu mkoani hapa kwa jina la Dunga umekutwa ukiningin'ia juu ya mti eneo la Daraja la Shani ambalo liko katikati ya Mji wa Morogoro.
Dunga aliwalipua maafande  zaidi ya sita ambao walihamishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema na yeye kuhamishwa mkoa wa Singida.
Hata hivyo, Dunga aligomea uhamisho huo akipinga watuhumiwa kutochukuliwa hatua.
Sababu alizotoa Dunga zinaelezwa katika barua aliyomwandikia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi aliyoitoa kwa mtandao huu na ambayo tunaichapisha.
(NA DUNSTAN SHEKIDELE,  GPL,  MOROGORO)