UTAFITI unaonyesha kuwa pamoja wasanii wa komedi yaani wachekeshaji
kuwa ni wasanii wasiokuwa na makuu katika maisha yao, lakini utata
umetanda katika malipo yao na maisha yao kwa ujumla, hivi karibuni kuna
mjadala umezuka katika vyombo vya habari vikielezea gharama za komedi
hizo kuwa chini katika utayarishaji.
FC imebaini kuwa baadhi ya watayarishaji wanavyotaka kuandaa filamu
uandaa bajeti ya lakini mbili tu kwa ajili ya malipo ya wasanii hiyo ni
kwa mtayarishaji asiye mchekeshaji wala hayupo karibu na wasanii wa
Komedi lakini kwa mchekeshaji kama ataamua kuandaa filamu lazima basi
anaweza kuandaa kuwaandalia washiriki Bangi, Gongo na ugali mkubwa.
Kwa mchekeshaji matata kidogo anaweza kununulia Bia na kuanza
kurekodi komedi husika, jambo ambalo baadhi ya wachekeshaji wamekiri
kutokea kwa jambo hilo huku wakidai kuwa baadhi ya wachekeshaji
hawajitambui jambo ambalo limefanya waandaaji kuwatumia kwa gharama
ndogo huku wakifanya kazi kubwa.
.
Wakati gharama za filamu hata mbovu uchukue kiasi cha milioni mbili
na na kwenda juu zaidi hali haipo hivyo katika Komedi, malipo ya msanii
mmoja ambaye hana jina ambayo ulipwa kwa kushiriki filamu kama malipo
utumika kutengenezea Komedi hadi kukamilika kwa ajili ya kuingia sokoni.
Msanii pekee ambaye analipwa malipo makubwa tofauti na wasanii
wengine ni Amri Athuman ‘King Majuto’ akifuatiwa na Salum Haji ‘Mboto’
na Mboto ameweza kulipwa malipo hayo kutokana na utengenezaji wake kuwa
ni tofauti kwani anawashirikisha wasanii wa filamu na si wachekeshaji.
Thamani ya komedi imeshuka sana katika malipo na hata wasanii, lakini
jambo ambalo wanatakiwa kujifunza ni kutoka kwa wasanii wenzao wa
Orijno Komedi ambao wameweza kujijengea utaratibu kuwa na kiwango
kikubwa cha malipo huku wakiweza kuwa na msimamo katika kulinda maslahi
yao.
Iwapo kama Komedi imerekodiwa na kukamilika kwa gharama ya laki sita
kwa kila kitu je Wasanii kama Senga, Dani na wengine walioshiriki
wamelipwa shilingi ngapi? Mpiga picha kalipwa shilingi ngapi? Mhariri
naye je? Uigizaji ni kazi kama zilivyo kazi nyingine kama msanii atakuwa
hajalipwa vema sanaa itaendelea kweli?
.
Kama ni kweli malipo ya kazi zenu ni Gongo, Bangi na Ugali mkubwa kwa
ngulu tafuteni staili nyingine ili maisha yaende hivi karibu Mzee king
Majuto alisema bora aachane na uigizaji hasa wa Komedi kwa sababu
wachekeshaji wanafanya utani yeye anauza Komedi moja kwa milioni nane
kumbe kuna komedi za lakini sita na zina nyota wengi!
Wasanii wa Komedi wanatakiwa kumshukru sana mkurugenzi wa Al Riyamy
Production ambaye kwanza amebadilisha mfumo wa komedi na kuweza
angalaukushindana na filamu japo si sana, siku za nyuma watayarishaji wa
Komedi walikuwa hawana bajeti wa mavazi lakini kwa sasa si haba,
Hongera Halfan Abdalah.