Wednesday, November 13, 2013

Promoter DMK aeleza kwa nini wasanii wa hip hop Bongo hawapati shows Marekani kama waimbaji, awashauri cha kufanya

Promoter DMK aeleza kwa nini wasanii wa hip hop Bongo hawapati shows Marekani kama waimbaji, awashauri cha kufanyaPromoter DMK, mtanzania anayefanya kazi ya kuwapeleka wasanii wa Afrika nchini Marekani na kuwaleta wamarekani Afrika, amesema wasanii wa bongo wanaofanya hip hop wanapata changamoto zaidi ya nafasi ya kupiga shows Marekani kwa sababu ya lugha wanayotumia na kwamba kule kuna watu wengi wanaofanya hip hop halisi.

DMK ambaye pia anamiliki kituo cha radio na TV ‘Swahili radio&TV’ kilichoko Marekani,  amefunguka katika kipindi cha ‘The Jump Off’ cha 100.5 Times fm alipokuwa akipiga story na Jabir Saleh, Dj D_Ommy na Dj K_U kuhusu fursa za wasanii wa bongo kupiga shows Marekani kupitia kampuni yake ya ‘DMK Global’.

“We unakuja unaimba hip hop halafu unaimba Kiswahili, ujue inakuwa kazi kidogo kwa sababu kule watu wanaimba hip hop na wanafanya ile yenyewe, sasa wewe unakuja unaimba Kiswahili inakuwa inasumbua kidogo.” Alisema DMK.

Promoter huyo aliwashauri wasanii wa Hip Hop kitu cha kufanya ambacho kitawawezesha kupiga shows Marekani na kukubalika pia.

“Sisi tunajaribu kidogo kuwaambia hawa wanamuziki wa hapa wapige muziki ambao uko commercial kidogo, kwa sababu muziki ni business sasa kama muziki ni business inabidi wacommercialize muziki wao.” Alisema DMK.