Monday, June 4, 2012

SUGU MOTO CHINI


Joseph Mbilinyi a.k.a Mr II a.k.a Sugu alionekana kujitabiria kifo cha umaarufu wake baada ya kufikia makubaliano na hasimu wake mkubwa Ruge Mutahaba. Kwa wafuasi wengi wa harakati za Anti-Virus, Sugu alionekana msaliti na wengi walitangaza kumpotezea kutokana na kitendo chake kukubaliana na adui yao. Hata hivyo tofauti na matarajio ya wengi, Sugu ameendelea kuwa SUGU baada ya kudhihirisha kuwa yeye bado ni kipenzi cha wanaburudani kwa Tanzania.

Show yake ya Usiku wa Sugu pale Dar Live ilijibu tuhuma zote baada ya kupanda jukwaani akiwa na Tshirt yenye nembo ya KINEGA kudhihirisha kwamba bado ni mwanachama halali wa movement ya Anti-Virus na pia bado ni mwanaharakati wa kutumainiwa katika muziki wetu wa Tanzania. Sugu aliambatana na Vinega wote toka movement ya Ant-virus hapa nazungumzia wasanii kama Mkoloni, Danny Msimamo, Suma Gee, pamoja na Mapacha ukipenda waite 'Magenge ya Mwenge'...Sugu ambaye ni mkali wa stage anayefanya ngoma zake zote live tofauti na wasanii wengi wa sasa, alionesha uwezo wa hali ya juu na pia alidhihirisha kwamba game ya zamani haiwezi kufa na milele itaendele kusimama.


Mashabiki wengi waliokuwa pale walikiri uwezo wa Sugu na kudai kwamba hakuna msanii mwenye uwezo kama wake. Sugu ambaye pia aling'arisha show ya Anti-Virus pale viwanja vya Ustawi wa Jamii amezidi kuonesha kuwa kuchana zaidi ya ngoma kumi live jukwaani inawezekana sio akina Jay Z peke yao ndo wanaweza. "Tatizo la wasanii wetu wa siku ukiwapa ngoma mbili live, utasikia sauti zinavyowakauka. Lakini huyu mchizi wa ajabu kinoma" shabiki mmoja alikuwa aking'aka baada ya show

Kivutio kingine kilichopamba show ya Sugu ni uwezo wa kimuziki aliouonesha mbunge mpya wa Arusha Mashariki kupitia chama cha CHADEMA, Mh Joshua Nassari. Mashabiki walimshangilia vya kutosha kuonesha kwamba wameukubali uwezo wake.