Mkurugenzi Mkuu wa Tamasha la Filamu za Majahazi Zanzibar (Zanzibar International Film Festival),Prof. Ikaweba Bunting (pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema leo asubuhi wakati wa kutangaza Ufunguzi rasmi wa Tamasha hilo ambalo linatarajiwa kuanza Julai 7 - 15 katika viwanja vya Ngome Kongwe Kisiwani Zanzibar.Tamasha hilo kwa Mwaka huu linatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mh. Dk. Ali Mohamed Shein huku Mgeni Maalum akitarajiwa kuwa Muongozaji wa Filamu kutoka Hollywood,Mario Van Peebles aliewahi kung'ara katika filau za American Most Wanted,New Jack City na nyingine nyingi.Wengine pichani ni Waratibu wa Tamasha hilo,kutoka kulia ni Muslim Nassor,Robert Monondoli na Sabrina Othman Faraji.
Mratibu wa Tamasha la Filamu za Majahazi Zanzibar (ZIFF),Muslim Nassor akionyesha picha ya Filamu iliyotengenezwa na Muongozaji wa Filamu kutoka Hollywood,Mario Van Peebles itakayopamba Tamasha hilo.Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Tamasha la Filamu za Majahazi Zanzibar(Zanzibar International Film Festival), Prof. Ikaweba Bunting