Sunday, July 1, 2012

MOJA YA AHADI YA JOHN MNYIKA ,KATA YA SINZA

  • Utekelezaji wa sehemu ya ahadi: ULINZI katika kata ya SINZA

    Katika miongoni mwa vipaumbele nane vilivyounda kifupi cha AMUA katika kampeni zangu mwaka 2010 ni suala la ULINZI katika Jimbo zima la Ubungo.

    Nashukuru leo 30.06.2012 kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali tumezindua kituo cha polisi katika kata ya Sinza.

    Uzinduzi uliohudhuriwa na wananchi, Mstahiki Meya wa Kinondoni, Yusuph Mwenda na Diwani wa Kata ya Sinza, Renatus Pamba.

    Natanguliza shukrani zangu za dhati sana kwa wananchi ambao tumeshirikiana katika mchakato huu, Diwani wa Kata ya Sinza, Renatus Pamba, Mstahiki Meya, Yusuph Mwenda (ambaye alichangia ujenzi wa kituo Sh milioni kumi (10)).

    Maslahi ya Umma Kwanza.

    John John MNYIKA
    Mbunge wa Jimbo la Ubungo (CHADEMA)
    30 Juni 2012