Serikali imesema itaanzisha mradi wa majaribio wa matibabu kwa kwa njia
ya mtandao (Telemedicine) kwa mwaka huu wa fedha ukishirikisha hospitali
mbalimbali nchini.
Akisoma
hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2012/13 ya
Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu bungeni leo, Waziri wa
Wizara hiyo, Profesa Makame Mbarawa alisema mpango huo utahusisha
Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) na hospitali mbalimbali
nchini.
Alitaja
hospitali hizo zitakazounganishwa na mtandao huo wa matibabu kuwa ni
Muhimbili, Amana, Temeke, Mwananyamala, Tumbi na Bagamoyo. Alisema
mpango huo utafanyika kwa kuihusisha Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na wadau wengine.