WEMA
Isaac Sepetu amelidokeza gazeti alipendalo la Ijumaa Wikienda kuwa
ameitwa ikulu ya Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza kwa mwaliko maalum.
Wema alisema mwaliko huo aliupata mara tu baada ya kuzindua ile filamu
yake ya Super Star wiki mbili zilizopita ambapo katika mwaliko huo wa
ujumbe kutoka ikulu hiyo ulimuomba kutoisambaza kwanza kabla ya kwenda
kuizindua nchini humo.
“Waliniambia juu ya mimi kuomba uraia wa nchi hiyo ili kukuza filamu
zao. Kusema kweli nilikuwa nina ratiba ya kwenda kuizindua filamu yangu
Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Yaani sijui hata
walijuaje. Sijui ni nini kimetokea, nina wasiwasi. Hata sijui nitaongea
nini na Rais wa Burundi,” alisema Wema na kuongeza kuwa maandalizi
yakikamilika atatii wito huo muda wowote