Friday, July 27, 2012

WEMA SEPETU NA DIAMOND MAPENZI YAO NI KAMA YA CHRIS BROWN NA RIHANNA


MSANII anayeongoza kwa ku-make headlines kwenye vyombo vya habari kila kukicha Wema Sepetu, amedai kuwa mahusiano yake yeye na mpenzi wake Nasseb Abdul ‘Diamond’, ni kama ya nyota wa marekaniRihanna na Chris Brown, huku akiamini kuwa kila kitu wanachokifanya kinakuwa kinafanana.


Wiki iliyopita Rihanna na Chris Brown, walioneka kwa nyakati tofauti huko St. Tropez, France wakila bata na kujiachia, ambapo hiyo pia imetokea kwa Wema na Diamond ambapo nao walionekana pamoja pande za Kigoma, Diamond alipoenda kwenye ziara ya Kigoma all stars inayoshirikisha wasanii wanaotokea mkoa wa kigoma.
Wema akiongea na DarTalk alidai kuwa hakuna mtu anayeweza kumfanya ashindwe kula bata na mpenzi wake huo kwani anaamini kwa kufanya hivyo ndiyo njia moja wapo ya kuwakata vilimi wale wanaozungumza mabaya juu ya mapenzi yao.
Hata hivyo mwandishi wa habari hizi, alitaka kujua mipango yao ya baadaye juu ya mapenzi yao ambapo alidai kuwa juu ya hilo hawezi kuzungumzia kwani ni miezi kadhaa walikuwa katika matatizo hivyo bado wanakula bata na watakapofikia maamuzi ya kuvishana tena pete watafanya hivyo.
“Mapenzi yetu hayana matatizo kwani wanadamu kutofautiana hiyo ni hali ya kawaida, hivyo sioni kama kuna haja ya kuongea sana, na kitendo cha sisi kuonekana pamoja sehemu za bata kuna watu inawauma na sisi hatujali kwani kila mtu ana maisha yake,” alisema Wema.
Mbali na ishu hiyo pia, mwandishi alitaka kujua tena itakuwaje kwa upande wa Jokate, alijibu kwa upande wake hamuoni kama ni mtu wa maana kwani mapenzi yake hakuna wa kukatisha ingawa anaamini Jokate ni mtoto mdogo sana kwake.
Chanzo Ni Blog ya Vijimambo