Sunday, August 5, 2012

Mkutano wa mtandaoni leo,juu ya marekebisho ya sheria ya hifadhi ya jamii

Mkutano wa mtandaoni leo, Saa saba mchana mpaka saa tisa alasiri. Changia maoni yako juu ya marekebisho ya sheria ya hifadhi ya jamii kurejesha fao la kujitoa. Ingia: http://www.mnyika.blogspot.com/ muda huo na uende ktk “comment” utoe maoni yako! Ni muhimu kuanza kupokea maoni na mapendekezo toka kwa wadau wa Hifadhi ya Jamii kabla ya kuwasilisha taarifa na muswada huo kwa Katibu wa Bunge kwa kuzingatia kuwa muswada huo nitauwasilisha kwa hati ya dharura. Wataarifu wengine!

Maslahi ya Umma kwanza