Friday, June 29, 2012

SERIKALI YASITISHA KUTOA TAMKO JUU YA MADAKTARI




Waziri Mkuu Mizengo Pinda

Waziri Mkuu Mizengo Pinda ametangaza kusitisha Serikali kutoa tamko lake kuhusu mgomo wa madaktari, ambao ulitakiwa kutolewa jana kama alivyoahidi juzi Bungeni.
Kauli hiyo imetolewa jana Bungeni na Waziri Mkuu, Pinda, alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mkuu wa Kambi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe, aliyetaka kujua Serikali ina mipango gani ya dharula ya kuumaliza mgomo huo.
Alisema kwa hivi sasa, Serikali imechukua dharura, kwa kuwaita madaktari wastaafu kwenda kwenye baadhi ya Hospitali za Serikali kushika nafasi maeneo ambayo madaktari waliogoma.
Vilevile Serikali imewataka wananchi waende kuhudumiwa kwenye hospitali za Jeshi, ikiwemo Lugalo.
Kuhusu Dkt Stephen Ulimboka, Mhe. Pinda ameseama kuwa hata yeye alipopokea taarifa kuwa Dkt. Ulimboka ametekwa na kupigwa na kwamba alisikitika sana, na anamuombea apone haraka ili waendelee na suluhisho la mgomo huo wa madakatari.
Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Mambo ya ndani kuunda jopo la wataalamu kuchunguza kwa haraka kuhusu tukio hilo.