Sunday, July 22, 2012

Mtoto wa Usher afariki dunia


Hatimaye mtoto wa kufikia wa Usher, Kyle Glover amefariki dunia, wiki mbili baada ya kujeruhiwa katika ajali ya boti.

Mtoto huyo wa mke wa zamani wa Usher, Tameka Foster amefariki jana asubuhi kwenye hospitali aliyokuwa amelazwa mjini Atlanta.

Kyle aligongwa na boti kichwani wakati akicheza kwenye ziwa Lanier kiasi cha kufanya ubongo wake ufe.

Kwa muda wote huyo mtoto huyo alikuwa amewekewa mashine maalumu ya kumsaidia kuishi.

Kabla ya ajali hiyo Usher, ambaye jina lake halisi ni Usher Raymond, alikuwa kwenye vita kali na mke wake huyo wa zamani ya kugombania watoto.

Salamu za rambirambi zimetolewa na mastaa mbalimbali kwenda kwa familia hiyo wakiwemo Justin Bieber, Toni Braxton Eric Benet na wengine.