Friday, July 27, 2012

WOLPER: NATAMANI KUZAA NA DALLAS


Jacqueline Wolper.
Na George Kayala
MKALI wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper amesema kuwa anatamani kuzaa na mchumba wake, Abdallah Mtoro ‘Dallas’ ifikapo mwaka 2015.
Akizungumza na Ijumaa juzikati, Wolper alisema anatambua ataolewa muda wowote na Dallas lakini atafurahi zaidi kama atapata mtoto akiwa na miaka 25.
“Natamani kupata mtoto nikiwa na umri wa miaka 25. Ninaye mchumba wangu Dallas ambaye najua atanioa muda wowote baada ya kuweka mambo sawa lakini pia nahitaji kuitwa mama haraka iwezekanavyo,” alisema Wolper.